Page 55 - Historia_Maadili
P. 55

Kazi ya kufanya 3.4


            Mapambano ya kupinga uvamizi wa kikoloni hayakuwa lelemama. Machifu
            na Watemi waliyapoteza maisha yao wakitetea maadili na ardhi yao isivamiwe
            na wageni. Soma matini kutoka vyanzo mbalimbali na uandike taarifa kuhusu
        FOR ONLINE READING ONLY
            viongozi walionyongwa kwa kuupinga uvamizi wa kikoloni.



          Mapambano ya Wahehe: Jamii ya Wahehe chini ya uongozi wa Mtwa Mkwawa
          (kama inavyoonekana kwenye Kielelezo 3.2), ilipinga vikali uvamizi wa Wajerumani
          kati ya mwaka 1891 na 1898 kwa njia ya vita. Kabla ya uvamizi huo, Wahehe
          walikuwa wamejiimarisha kibiashara kwa kudhibiti maeneo mengi. Sababu kubwa
          ya mapambano ya Wahehe dhidi ya Wajerumani ilikuwa kuyalinda maadili, uhuru
          na masilahi yao, hasa ya kiuchumi. Kwa mfano, katika jitihada za kujiimarisha
          kiuchumi, Wahehe walipanua maeneo yao hasa sehemu za Mpwapwa na Usagara ili
          kuongeza kipato kupitia ushuru waliotoza kwa misafara ya wafanyabiashara waliopita
          katika eneo lao kutoka Bagamoyo kwenda bara huko Tabora, Ujiji, kanda ya Ziwa
          na Katanga.

          Kwa upande wao, Wajerumani walikuwa wanapanua himaya yao kuelekea bara
          na walikasirishwa na kitendo cha Wahehe kuendelea kujiimarisha kwa kuongeza
          maeneo kama Usagara, Mpwapwa na Ugogo. Kuimarika kwa himaya ya Wahehe
          kulisababisha Wajerumani kukosa mapato ya ushuru na malighafi kutoka bara. Aidha,
          Wahehe walikuwa wanaendeleza nguvu zao kutoka Kalenga, ambayo ilikuwa ngome
          ya Mtwa Mkwawa hadi maeneo mengine.

          Wahehe walipendelea kumaliza mzozo wao na Wajerumani kwa njia ya mazungumzo
          ya amani, hivyo Mkwawa alituma askari wawili kupeleka ujumbe kwa kiongozi wa
          Wajerumani huko pwani. Hata hivyo, Wajerumani walihisi askari hao walikuwa
          wapelelezi na hivyo waliwaua. Kitendo hiki cha kikatili kilimkasirisha sana Mtwa
          Mkwawa na ndipo alipoamua kuanzisha mapambano rasmi dhidi ya Wajerumani.

          Mapambano ya kwanza ya kijeshi kati ya Wahehe na Wajerumani yalifanyika mwaka
          1891 katika eneo la Lugalo. Wanajeshi wa Kijerumani chini ya uongozi wa kamanda
          Emil von Zelewisky (aliyejulikana kwa jina la Nyundo), walitumwa kuangamiza
          Wahehe. Katika mapigano hayo, wapiganaji wa Kihehe waliwashinda Wajerumani
          na askari 300 wa Kijerumani pamoja na kiongozi wao waliuawa. Kaburi la kiongozi
          huyo wa Kijerumani bado lipo katika eneo la Lugalo, mkoani Iringa, hadi leo.
          Kielelezo 3.3 kinaonesha mnara wa kumbukumbu walipouwawa askari wa Kijerumani
          wakiongozwa na Emil Zelewisky huko Lugalo Iringa mwaka 1891.

                                                  47




                                                                                        03/10/2024   18:15:13
   HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd   47
   HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd   47                                         03/10/2024   18:15:13
   50   51   52   53   54   55   56   57   58   59   60