Page 53 - Historia_Maadili
P. 53
Zoezi la 3.2
1. Je, ni sababu gani ziliwafanya jamii za Kitanzania kupinga utawala wa
kikoloni?
2. Eleza mbinu ambazo jamii za sasa za Kitanzania zinaweza kutumia
FOR ONLINE READING ONLY
kulinda rasilimali, utamaduni na maadili ya jamii zao.
3. Jadili namna maadili ya Watanzania yaliyokiukwa kutokana na uvamizi
wa kikoloni.
4. Fafanua athari za kiuchumi kwa jamii za Kitanzania zilizosababishwa na
utawala wa kikoloni.
Upinzani dhidi ya uvamizi wa kikokoni katika jamii za Kitanzania
Karibu jamii zote za Kitanzania ziliupinga uvamizi wa kikoloni kwa sababu hakuna
jamii iliyopenda kuupoteza uhuru na utamaduni wake kwa wageni. Jinsi jamii hizi
zilivyoupinga uvamizi huo, au njia gani walizozitumia zilitegemea uwezo wa kivita,
kiuchumi, mazingira na uongozi bora na imara. Kwa hiyo, kuna jamii zilizoupinga
ukoloni kwa kupigana vita, zingine kwa kujisalimisha na nyingine kwa kuungana
na wavamizi.
Njia ya kupambana kwa vita
Njia ya vita ilikuwa maarufu zaidi kati ya jamii za Kitanzania, kwani jamii nyingi
hazikuwa tayari kuupoteza uhuru wao na hivyo ziliupinga waziwazi uvamizi huo
kwa kutumia vita. Jamii hizi nyingi zilikuwa na uongozi shupavu, zilimiliki silaha,
zilikuwa na uwezo wa kiuchumi na nyingi pia zilikuwa chini ya dola zenye nguvu.
Mapambano dhidi ya uvamizi yalihusisha jamii moja moja au jamii nyingi kwa
pamoja. Kwa mfano, mapambano ya mwanzo dhidi ya uvamizi wa kikoloni na maadili
yake yalihusisha jamii moja moja na siyo makabila mengi au nchi nzima.
Mapambano ya Wanyamwezi: Harakati za kuupinga uvamizi wa kikoloni magharibi
mwa Afrika Mashariki ya Kijerumani, ziliongozwa na Mtemi wa Wanyamwezi
aliyejulikana kama Isike au Mwana Kiyungi kuanzia mwaka 1886 hadi 1891. Mtemi
Isike alipinga vikali uvamizi wa Wajerumani katika himaya yake baada ya maeneo
yake ya kiutawala kuporwa. Pia, alitetea masilahi ya biashara iliyokuwa ikifanyika
miongoni mwa jamii ya Wanyamwezi huko Tabora. Mtemi Isike alikusanya ushuru
kutoka kwa wafanyabiashara wa Kiarabu waliokuwa wakipita katika himaya yake
kuelekea Ujiji mpaka Katanga (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo), Burundi
na wengine kaskazini kuelekea kanda ya Ziwa Viktoria hadi ufalme wa Buganda na
Bunyoro.
45
03/10/2024 18:15:12
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 45
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 45 03/10/2024 18:15:12

