Page 58 - Historia_Maadili
P. 58

Liti na askari wake walipambana na  Wajerumani  mara mbili na kufanikiwa
          kuwakimbiza nje ya mji wa Singida kwa kutumia mbinu ya kipekee ya silaha ya
          nyuki wakali.  Wakati vita vilipokuwa
          vikipamba moto, nyuki hao walifunguliwa
          na kuwashambulia Wajerumani pekee na
          askari wao. Mapambano kati ya Liti na
        FOR ONLINE READING ONLY
          Wajerumani yalidumu kwa miaka mitatu,
          kuanzia mwaka 1908 hadi 1910.

          Hata hivyo, katika jaribio la tatu na la
          mwisho, Liti hakufanikiwa kuwashinda
          Wajerumani kutokana na kusalitiwa
          na mmoja wa washirika wake. Hivyo,
          Wajerumani walimkamata yeye na mume
          wake, Nyalandu Mtinangi na kuwaua.
          Kichwa cha shujaa huyu kilikatwa na
          kupelekwa Ujerumani. Kielelezo 3.6              Kielelezo 3.6:  Liti Kidanka
          kinaonesha picha ya Liti Kidanka.

          Hii ni mifano michache ya mapambano ya kuupinga uvamizi wa kikoloni kwa njia
          ya vita yaliyofanywa na makabila moja moja. Zaidi ya hayo, jamii za Kitanzania
          zilitumia njia ya vita kupinga mfumo wa ukoloni na hasa uchumi wa kikoloni kwa
          kushirikisha makabila mengi. Hata hivyo, ni muhimu kufahamu kuwa makabila haya
          yalipigana kila moja kivyake. Mfano mzuri wa aina hii ya mapambano ya kushirikisha
          makabila mengi ni Vita ya Maji Maji.

          Mapambano ya jamii za Kusini mwa Afrika Mashariki ya Kijerumani: Mapambano
          ya jamii za kusini, yajulikanayo kama Vita vya Maji Maji, yalianza mwaka 1905 na
          kumalizika mwaka 1907. Kiongozi wa mapambano haya alikuwa Kinjekitile Ngwale
          wa kabila la Wamatumbi, ambaye aliwaongoza Wamatumbi kupinga ukatili, unyonyaji
          na ukandamizaji wa Wajerumani. Kinjekitile alikuwa kama roho ya mapambano hayo
          na aliwaahidi kuwalinda wafuasi wake dhidi ya Wajerumani.

          Alidai kuwa ameoteshwa dawa ambayo ingewaepusha na risasi za wavamizi. Dawa
          hiyo ilikuwa ni maji yaliyochanganywa na mtama, yaliyodaiwa kuwa na uwezo wa
          kuzigeuza risasi kuwa maji. Wanajamii waliamini ahadi zake na, hata vita vilipoanza,
          wakoloni waliporusha risasi, wao walitamka “maji.” Hata hivyo, kadri walivyosema
          “maji,” ndivyo walivyopoteza maisha. Vita hivi vilienea katika maeneo ya kusini na
          mashariki mwa Afrika Mashariki ya Kijerumani, kama vile Rufiji, Mohoro, Somanga,
          Kibata, Nandete, Mikindani, Liwale, Lindi, Songea, Njombe na Mahenge. Kinjekitile
          alitumia mbinu hii ili kuwaunganisha na kujenga mshikamano miongoni mwa
          wananchi ili wapambane na mkoloni bila hofu. Angalia Kielelezo 3.7 kinachoonesha
          baadhi ya jamii zilizopinga utawala wa Wajerumani.

                                                  50




                                                                                        03/10/2024   18:15:13
   HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd   50                                         03/10/2024   18:15:13
   HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd   50
   53   54   55   56   57   58   59   60   61   62   63