Page 56 - Historia_Maadili
P. 56
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo 3.2: Mtwa Mkwawa Kielelezo 3.3: Mnara wa kumbukumbu
walipouwawa askari wa Kijerumani
Licha ya kushindwa mwaka 1891, Wajerumani waliendelea kujiimarisha kivita
kwa kuanzisha vikosi vya kijeshi katika maeneo ya Kilosa na Kisaki. Baada ya
kujiimarisha, Wajerumani walituma wajumbe kwa Mtwa Mkwawa wakimtaka
aitambue serikali ya Wajerumani, alipe gharama za vita, aache kuvamia misafara ya
kibiashara katika maeneo jirani na utawala wake, asalimishe silaha zilizotekwa na
aruhusu wafanyabiashara na wamisionari kutumia eneo lililokuwa chini ya utawala
wake. Mkwawa alikataa mapendekezo yote hayo, akipinga ukatili, unyonyaji na
unyanyasaji uliokuwa unafanywa na Wajerumani.
Mwaka 1894, Wajerumani chini ya Kamanda Tom Prince walivamia ngome ya
Wahehe huko Kalenga. Mkwawa alikimbilia mafichoni na kuendelea na vita vya
msituni. Mwaka 1898, Mtwa Mkwawa aliamua kujiua badala ya kukamatwa na
Wajerumani. Kifo cha namna hii kilikuwa ushujaa wa aina yake, kwani Mkwawa
aliona ni fedheha kwa shujaa kukamatwa, kunyanyaswa na kuuawa kikatili kwa
kunyongwa na wavamizi.
Mapambano ya Wayao: Mapambano ya kupinga uvamizi wa Wajerumani upande
wa kabila la Wayao yaliongozwa na kiongozi wao jasiri na shupavu, Mwene
Machemba. Mwene Machemba alishinda karibu mapigano yote aliyoyaongoza dhidi
ya Wajerumani. Ushindi huu ulitokana na ukweli kwamba Mwene Machemba alikuwa
kiongozi hodari, shupavu na mwenye kupenda kutetea maadili na uhuru wa watu
wake. Kwa mfano, katika barua aliyowaandikia Wajerumani, Mwene Machemba
48
03/10/2024 18:15:13
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 48 03/10/2024 18:15:13
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 48

