Page 57 - Historia_Maadili
P. 57
alisema: “Nimesikiliza maneno yenu, lakini sijaona
sababu ya kuwatii. Niko tayari kufa…, sisemi mnitii
mimi kwa kuwa nyie ni watu huru kama mimi.”
Maneno haya yanaonesha jinsi alivyosimamia utu
na uhuru wa watu wake kwa ujasiri mkubwa.
FOR ONLINE READING ONLY
Hata hivyo, Mwene Machemba alikimbilia
Msumbiji baada ya kupambana vikali na majeshi
ya Wajerumani, ambapo Wayao walizidiwa nguvu
na kushindwa vita. Kielelezo 3.4 kinaonesha picha
ya Mwene Machemba. Kielelezo 3.4: Mwene Machemba
Mapambano ya Wachaga: Mapambano dhidi ya uvamizi wa Wajerumani katika jamii
ya Wachaga yaliongozwa na viongozi wa Kibosho na Moshi. Kwa upande wa Kibosho,
wakiwa chini ya uongozi wa Mangi Sina, walipinga kitendo cha Wajerumani kuingilia
mgogoro uliokuwepo miongoni mwa watawala wa Kibosho, Moshi na Marangu.
Kitendo hicho kilimuudhi Mangi Sina, kwani kilionekana kuwa na nia ya kuwagawa.
Kwa hasira, Mangi Sina aliichana bendera ya Wajerumani, kitendo ambacho kilikuwa
ishara ya kuupinga ukatili na unyanyasaji uliokuwa unafanywa na Wajerumani
Uchagani. Kitendo hicho kiliwakasirisha Wajerumani, ambao walituma majeshi ya
kukodi ya Wanubi kutoka Sudani ili kupambana naye. Hata hivyo, baada ya kuzidiwa
nguvu na majeshi ya Wajerumani, Mangi Sina alilazimika kutoroka.
Vilevile, Mangi Meli aliongoza mapambano dhidi
ya Wajerumani huko Moshi, akipinga ukatili na
mfumo wa unyanyasaji na unyonyaji wa wakoloni.
Katika mapambano hayo, kamanda wa jeshi la
Wajerumani, Von Bulow, aliuawa. Kwa kulipiza
kisasi, Wajerumani walimshambulia Mangi Meli,
wakamkamata na baadaye wakamnyonga kwa ukatili
kijijini kwake. Kielelezo 3.5 kinaonesha picha ya
Mangi Meli.
Kielelezo 3.5: Mangi Meli
Vita vya Liti Kidanka dhidi ya Wajerumani (1908-1910): Wajerumani walifika Singida
mnamo mwaka 1901. Wajerumani walikabiliana na upinzani mkali kutoka kwa
Wanyaturu, walioongozwa na mwanamke shupavu, Liti Kidanka, kupinga uvamizi
huo. Liti Kidanka hakutaka Wajerumani watawale eneo ambalo sasa ni Mji wa Singida.
Hivyo, aliongoza mapambano makali dhidi ya askari wa Kijerumani walioongozwa
na Kapteni Eberhard von Sick.
49
03/10/2024 18:15:13
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 49 03/10/2024 18:15:13
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 49

