Page 59 - Historia_Maadili
P. 59
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo 3.7: Jamii zilizopinga utawala wa Wajerumani
Kazi ya kufanya 3.5
Kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya taarifa ikiwemo mitandao andika nukuu
ya Mwene Machemba kwenye barua aliyowaandikia Wajerumani, kisha eleza
jinsi alivyopinga uvamizi kwa nguvu zake zote.
Kwa njia ya kuungana
Kuna jamii za Kitanzania zilijua nguvu ya kijeshi ya Wajerumani na hawakuwa tayari
kupambana na kuupinga uvamizi wao moja kwa moja. Lakini waliungana ili kuweza
kuwashinda maadui wao. Hii ilitokana na imani kwamba, baada ya kuwashinda
maadui wao wa muda mrefu wangebaki kuwa na nguvu zaidi na kujiimarisha. Pia,
kuungana huku walikusudia kupata misaada ya silaha na vifaa vingine kutoka kwa
Wajerumani. Silaha na vifaa hivyo vingewafanya kuwa imara zaidi hata kuwashinda
51
03/10/2024 18:15:14
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 51
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 51 03/10/2024 18:15:14

