Page 51 - Historia_Maadili
P. 51
Mapambano haya yalilenga kuzuia kuingizwa kwa maadili ya kikoloni katika jamii za
Kitanzania. Jamii hizi zilikuwa na maadili, mila na desturi zilizowiana na mazingira
yao, pamoja na lugha, ngoma na imani za kidini (dini za jadi). Kila jamii ilikuwa na
imani katika Mungu, ambaye alitambulika kwa majina mbalimbali ya kijadi kama vile
Mlungu, Mnungu (kwa Wazigua), Kyala (kwa Wanyakyusa), Ruwa (kwa Wachaga)
na Ngai (kwa Wamasai).
FOR ONLINE READING ONLY
Hata hivyo, baada ya kuingia kwa wakoloni na kuanzisha utawala wao, utamaduni na
maadili ya jamii za Kitanzania yalidhoofishwa na kutajwa kuwa ya kishenzi. Wakoloni
walileta utamaduni kutoka katika mataifa yao uliosisitiza maadili ya kibepari, ikiwa
ni pamoja na ubaguzi wa rangi, uporaji, ukatili, unyonyaji, unyanyasaji, matabaka na
ubinafsi. Pia, walileta maadili ya dini za kigeni (Ukristo na Uislamu) ambayo mara
nyingi yalipingana na maadili ya dini za jadi.
Kazi ya kufanya 3.1
Soma matini kutoka vyanzo mbalimbali na ubainishe tofauti ya uvamizi
uliokuwepo kati ya Afrika Mashariki ya Kijerumani (Tanganyika) na Zanzibar.
Kazi ya kufanya 3.2
Kwa kutumia taarifa kutoka vyanzo mbalimbali fanya uchunguzi kuhusu Karl
Peters alivyoingia mikataba ya kilaghai. Andika insha yenye maneno mia tatu
(300) ukiwashauri viongozi wa kizazi cha sasa kipi cha kujifunza kutokana na
mikataba ya Karl Peters.
Zoezi la 3.1
1. Eleza dhana ya mtawala na mtawaliwa.
2. Tofautisha utawala wa Waarabu Zanzibar na ule wa Wajerumani katika
Afrika Mashariki ya Kijerumani.
3. Fafanua mbinu zilizotumiwa na wakoloni kuanzisha utawala wa kikoloni
Tanganyika.
4. Eleza namna maadili ya kibepari yanavyoendelea kuathiri maadili ya jamii
za Kitanzania wakati wa sasa.
43
03/10/2024 18:15:12
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 43 03/10/2024 18:15:12
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 43

