Page 48 - Historia_Maadili
P. 48
ya Majimaji, iliyopiganwa kuanzia mwaka 1905 hadi 1907. Vilevile, nyimbo hizi
zilitumika kuwahamasisha na kuwaunganisha wapiganaji dhidi ya majeshi ya kikoloni
ya Wajerumani.
Kadhalika, utamaduni wa masimulizi ulisaidia kueneza elimu kwa vizazi vichanga
kuhusu maadili, kanuni za kijamii na stadi maisha. Wakati wa ukoloni, mifumo
FOR ONLINE READING ONLY
rasmi ya elimu ilidhibitiwa na wakoloni, hivyo jamii zilihakikisha kwamba watoto
wa Kitanzania wanaendelea kujifunza utamaduni na historia yao kupitia kwa wazee.
Kwa mfano, miongoni mwa jamii za Wanyamwezi, wazee walisimulia hadithi ili
kutoa mafunzo kuhusu ushujaa, hekima na umuhimu wa jumuiya, ambayo yalikuwa
muhimu katika kusaidia jamii kukabiliana na changamoto za utawala wa kikoloni.
Zoezi la 2.5
1. Kwa nini wakoloni walishindwa kutokomeza maadili ya Kitanzania pamoja
na jitihada kubwa walizozifanya?
2. Eleza umuhimu wa masimulizi katika kuyadumisha maadili ya Kitanzania.
3. Bainisha maadili mengine ya jamii za Kitanzania yaliyodumu licha ya
ushawishi wa utawala wa kikoloni kuyafuta.
4. Eleza mchango wa serikali ya Tanzania katika kuenzi na kudumisha maadili
ya Kitanzania.
Mavazi: Jamii za Kitanzania ziliendelea kuenzi mavazi yao ya kiasili hata katika
kipindi cha ukoloni. Jamii mbalimbali zilichukua juhudi za kipekee kuendeleza na
kusambaza maarifa ya mavazi ya jadi kwa vizazi vilivyofuata, zikitambua umuhimu
wa kuheshimu na kudumisha utamaduni wao wa kipekee licha ya shinikizo kubwa la
kuvaa mavazi tofauti yaliyoletwa na wageni. Mavazi ya Ulaya Magharibi yalijenga
taswira ya ubora wa utamaduni wao, imani mpya, nguvu, ustaarabu na usomi. Mavazi
ya asili yalienziwa kupitia matamasha, mikusanyiko na sherehe mbalimbali za kijadi
kama vile sherehe za mavuno, jando na unyago, harusi na tohara.
Kazi ya kufanya 2.5
Fanya utafiti katika jamii unamoishi na bainisha maadili ya jamii za Kitanzania
yaliyokuwepo wakati wa ukoloni ambayo bado yanaenziwa hadi wakati wa sasa.
40
03/10/2024 18:15:11
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 40
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 40 03/10/2024 18:15:11

