Page 43 - Historia_Maadili
P. 43
Mavazi: Baada ya ujio wa ukoloni, kulianza kujitokeza mabadiliko ya taratibu katika
mitindo ya mavazi. Mavazi ya Kimagharibi kama vile suti, tai, magauni, kaptula,
suruali na mengineyo, yalianza kuingizwa na kukubalika, hasa miongoni mwa
walioelimika au wale waliokuwa na ushawishi katika utawala wa kikoloni. Hii
ilisababisha kudunishwa au kupuuzwa kwa mavazi na maadili ya kijadi ya mavazi.
Mabadiliko haya mara nyingi yalisababisha kuachwa
FOR ONLINE READING ONLY
kwa mavazi ya kiutamaduni, kwani mitindo ya
Kimagharibi ilihusishwa na usasa, maendeleo, ustaarabu,
nguvu za utawala na heshima. Pia, maadili na tabia za
jamii zilianza kubadilika kutokana na ushawishi wa
utamaduni wa kigeni wa mavazi.
Vilevile, katika maeneo ya pwani, hasa miongoni
mwa jamii za Waswahili, mavazi yaliathiriwa sana
na utamaduni wa Kiarabu kutokana na karne nyingi
za biashara na mwingiliano. Kwa kawaida, wanaume
wa Kiarabu huvaa “kanzu,” vazi refu ambalo mara
nyingi huwa na rangi nyeupe, huku wanawake wakivaa
“baibui” vazi jeusi linalofunika mwili mzima. Mavazi
ya Waswahili kwa kiasi kikubwa yaliakisi utamaduni
wa Kiarabu. Vielelezo 2.3 na 2.4 vinaonesha baadhi ya Kielelezo 2.3: Vazi la baibui
mavazi yaliyoletwa na wageni.
Kielelezo 2.4: Vazi la suti na kanzu
35
03/10/2024 18:15:11
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 35 03/10/2024 18:15:11
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 35

