Page 47 - Historia_Maadili
P. 47
Ukarimu: Jamii za Kitanzania zilijulikana kwa ukarimu wao na thamani hii
iliendelezwa hata wakati wa ukoloni. Jamii hizi ziliamini katika umuhimu wa
kuwatendea wageni kwa heshima na ukarimu. Pia, jamii hizi ziliendelea kusisitizwa
kuonesha uvumilivu na utu katika kuishi na kushirikiana na watu wa tamaduni
tofauti, huku wakijifunza na kuchangamana nao. Thamani ya umoja na mshikamano
ilisisitizwa katika kukabiliana na changamoto za ukoloni, kihistoria na kiuchumi,
FOR ONLINE READING ONLY
ambapo jamii hizi zilipigania uhuru na haki ya kujitawala.
Utii kwa mamlaka: Wakati wa utawala wa kikoloni, heshima kwa uongozi wa ndani
na miundo ya kimila iliendelea kudumishwa. Heshima hii ilienea pia kwa watawala wa
kikoloni, ingawa mara nyingi iliambatana na upinzani. Kwa mfano, chini ya utawala
wa kikoloni, jamii nyingi za Kitanzania ziliendelea kuwaheshimu viongozi wao wa
kimila kama machifu, wazee na wakuu wa koo. Viongozi hawa walionekana kama
mamlaka halali zinazosimamia masilahi ya jamii. Kwa mfano, jamii za Wachaga na
Wahehe ziliendelea kuwaheshimu machifu wao, ambao walijulikana kama Mangi
na Mtwa mtawalia, kama viongozi wao halali. Licha ya kuwepo kwa watawala wa
kikoloni, jamii nyingi za Kitanzania mara nyingi zilishauriana na machifu wao katika
kutoa uamuzi na miongozo mbalimbali. Hali ambayo ilidhihirisha heshima kwa
mifumo yao ya utawala wa kimila.
Utamaduni wa masimulizi: Uwasilishaji wa historia, utamaduni na maadili kupitia
masimulizi, hadithi, mashairi, methali na nyimbo ulibaki kuwa njia muhimu ya
kuhifadhi historia na utambulisho wa makabila/jamii mbalimbali za Kitanzania.
Maadili haya yalikuwa muhimu kwa mifumo ya jamii za Kitanzania. Hii ilisaidia
kudumisha utambulisho na mwendelezo hata chini ya utawala wa kikoloni. Simulizi
hizi zilikuwa na mchango mkubwa katika kuhifadhi historia, maadili na imani za
jamii za Kitanzania na zilizuia rekodi hizi kupotoshwa na wakoloni.
Vilevile, mapokeo ya simulizi yaliwezesha jamii kudumisha utambulisho wao kwa
kurithisha hadithi, methali, nyimbo, utani na ngano ambazo zilikuwa na urithi wao
wa kitamaduni. Kwa mfano, hadithi kuu za Wasukuma, ambazo zilirithishwa kutoka
kizazi kimoja hadi kingine, zilibeba kumbukumbu ya hekima na ujasiri wa mababu zao
na zilitumika kama chanzo cha fahari na utambulisho, hata wakati ambapo wakoloni
walijaribu kukandamiza tamaduni za wenyeji.
Aidha, utamaduni wa masimulizi ulichangia kueneza hisia za kupinga ukoloni. Kwa
mfano, hadithi na nyimbo zilitumika kukosoa mamlaka za kikoloni, kutia moyo
ujasiri na kukuza mshikamano miongoni mwa wanyonge. Mathalani, nyimbo na
ngoma miongoni mwa jamii za Wangoni waliopo kusini mwa Tanzania zilijumuisha
ujumbe wa upinzani dhidi ya majeshi ya kikoloni ya Wajerumani wakati wa Vita
39
03/10/2024 18:15:11
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 39 03/10/2024 18:15:11
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 39

