Page 42 - Historia_Maadili
P. 42
ustaarabu ulianza kupimwa kwa kujua lugha za kigeni na utamaduni wa kikoloni
kama lugha, mavazi, aina ya vyakula na kazi za ofisini na utawala.
Aidha, ukoloni ulisababisha kutengenezwa kwa vitabu na nyaraka nyingi kwa lugha
za kikoloni badala ya lugha za asili, hivyo kusababisha upungufu wa vyanzo vya
maarifa kwa lugha za asili za Tanzania. Hii ilisababisha watoto kujifunza masomo
FOR ONLINE READING ONLY
yao yote kwa lugha za kigeni na hivyo kupoteza uwezo wao wa kujieleza vizuri
kwa lugha zao za asili. Kama inavyoaminika na wataalamu wengi wa elimu, hali hii
iliwafanya wanafunzi wapoteze uwezo wao wa ubunifu, kuelewa na kujiamini, kwa
sababu lugha waliyoitumia haikuwa ya asili yao. Hata hivyo, kwa Tanzania, ukoloni
ulitumia lugha ya Kiswahili kwa shughuli za Waafrika kama kutoa maelekezo na
kendesha kesi katika mahakama za wenyeji zilizosimamiwa na machifu.
Zaidi ya hayo, mifumo ya elimu ya kikoloni ilisababisha kuibuka kwa msamiati
wa kigeni. Kwa mfano, maneno mengi ya Kiingereza na Kijerumani yalipokelewa,
kutoholewa na kutumika katika Kiswahili. Mfano wa maneno haya ni “shule” kutoka
“schule,” “nanasi” kutoka “ananas,” na “hela” kutoka “heller” yalitoka katika
lugha ya Kijerumani. Pia, maneno kama “polisi” kutoka “police,” “benki” kutoka
“bank,” “baiskeli” kutoka “bicycle,” na “hospitali” kutoka “hospital” yalitoka katika
lugha ya Kiingereza. Vilevile, athari za lugha za kikoloni zimejidhihirisha kupitia
maneno, misemo na mabadiliko ya sarufi. Mabadiliko haya yanaonesha jinsi ukoloni
ulivyoweza kubadilisha matumizi ya lugha za Kitanzania na kuathiri utamaduni na
mawasiliano ya kila siku.
Katika kipindi cha 1890-1961, Kiswahili kiliathiriwa sana na kuingiliana na lugha za
kikoloni. Ushawishi wa kikoloni, kama vile Wajerumani, ambao walikuwa wakoloni
wa kwanza nchini ulijidhihirisha kupitia matumizi ya lugha ya Kijerumani kwenye
baadhi ya masuala ya utawala na kidogo sana kwenye elimu. Baadaye, Waingereza
walipochukua mamlaka baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, Kiingereza kilitumika
kama lugha ya kufundishia shuleni na lugha rasmi ya serikali.
Kazi ya kufanya 2.4
Andika insha isiyopungua maneno 200 ukionesha:
(a) Umuhimu wa kuhifadhi na kuendeleza lugha za asili kwa jamii za
Kitanzania; na
(b) Mikakati ya kuhifadhi na kuendeleza lugha za asili kwa kizazi cha sasa
na kijacho.
34
03/10/2024 18:15:11
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 34
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 34 03/10/2024 18:15:11

