Page 40 - Historia_Maadili
P. 40
magonjwa. Vilevile, huduma za afya za jadi zilihusishwa na imani za jadi, ambapo
matambiko yalifanyika kutibu baadhi ya magonjwa.
Ujio wa wakoloni ulileta mabadiliko makubwa katika mfumo wa afya, kwani
walianzisha hospitali na vituo vya afya katika maeneo mbalimbali nchini kwa kutumia
mtindo na mfumo wa Ulaya magharibi. Walileta pia dawa mbalimbali za kutibu
FOR ONLINE READING ONLY
magonjwa ambazo zilikuwa tofauti na zile za asili zilizotumika kabla ya ukoloni.
Aidha, wakoloni walibeza na kudunisha mfumo wa tiba za asili kwa kutumia mbinu
mbalimbali kama vile dini, kugawa dawa za kimagharibi kwa jamii za Kitanzania na
kueneza propaganda kuwa tiba za asili hazina msaada wowote, ni uchawi na ushirikina
na ni alama ya umasikini na ukosefu wa maendeleo. Zaidi ya hayo, serikali ya kikoloni
ilizuia na kuwakamata wataalamu wa tiba za asili, hatua ambayo iliathiri kwa kiasi
kikubwa imani na maadili ya mfumo wa afya wa jadi. Ukweli unabaki kuwa dawa za
Ulaya magharibi pia zilitokana na mimea na wanyama kama za Waafrika ila wazungu
walizichakata viwandani, kuzifungasha katika vifungashio na waliziwekea vipimo
maalumu ili kutibu ugonjwa unaohusika.
Athari za kiutamaduni
Ujio wa wakoloni ulileta athari mbalimbali za kiutamaduni kwa jamii za Kitanzania
kama inavyoelezewa hapa chini.
Dini za jadi: Kabla ya kuja kwa dini za kigeni kama Ukristo na Uislamu, jamii
za Kitanzania zilikuwa na imani za kiasili zilizokita mizizi katika utamaduni wa
jamii iliyohusika. Dini hizi mara nyingi zilihusisha ibada za kuabudu Mungu kupitia
miungu, mababu na mizimu katika maeneo mbalimbali kama vile mapango, mito,
mabwawa, milima, majabali makubwa na miti mikubwa. Imani za dini za jadi zilijikita
katika kulinda na kudumusha maadili mema ya jamii.
Ujio wa ukoloni nchini uliathiri na kuleta mifumo mipya ya imani na dini, ambayo
iliendana na utamaduni wa Ulaya Magharibi. Kwa mfano, wamisionari wa Kikristo
walileta mafundisho mapya yenye mila, desturi na maadili mapya, huku wakilenga
kubadilisha imani za jamii za Kitanzania. Aidha, dini za jadi za Kitanzania
zilidharauliwa na kupigwa vita na wakoloni kama sehemu ya juhudi zao za kueneza
mila na desturi za nchi za Ulaya Magharibi. Hii ilisababisha jamii nyingi za Kitanzania
kuukubali mfumo wa dini za Kikristo na hivyo kuwa na maadili ya Ulaya Magharibi
au maadili mseto. Maadili ya asili yalishambuliwa kuwa si bora, yaliwakandamiza,
kuwabagua na kuwadunisha wanawake. Hivyo maadili ya asili yalipata mtikisiko
mkubwa kutoka kwenye imani hii mpya ya Kikristo.
Kwa ujumla, imani za asili zilichukua sura mpya, zikichanganywa na mafundisho ya
Kikristo na utamaduni wa wakoloni. Matokeo yake, dini ya Kikristo ilipata msukumo
32
03/10/2024 18:15:10
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 32 03/10/2024 18:15:10
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 32

