Page 35 - Historia_Maadili
P. 35
dhidi ya maadui wa ndani na nje. Mteko alikuwa kiongozi msaidizi wa jeshi. Pia,
alikuwa mkuu wa huduma za siri na ujasusi. Kikoma alikuwa mkuu wa habari na
Minule alikuwa mkuu wa kukusanya kodi katika misafara iliyopita katika eneo la
Unyanyembe.
Sheria na kanuni za kijadi ziliweka maadili na miongozo kuhusu ushirikiano, haki na
FOR ONLINE READING ONLY
nidhamu. Familia zilikuwa ndio msingi wa jamii na watu walihusishwa na familia
zao pana, ikijumuisha koo au ukoo. Mfumo wa ukoo ulikuwa na umuhimu mkubwa,
ambapo jamii nyingi zilikuwa na mifumo ya kikabila na kiukoo iliyosimamia na
kuratibu masuala muhimu kama ndoa, rasilimali, urithi, jando na unyago, pamoja na
tiba za asili. Vilevile, mfumo wa miiko ulisimamia matendo mema kama vile heshima,
ukarimu, upendo, uadilifu na uzalendo.
Pia, sheria za kijadi zilisimamia mienendo ya watu na zilitekelezwa na wazee wa
kimila. Sheria hizi zilitungwa kwa misingi ya haki, usawa na kulinda masilahi ya jamii
nzima. Adhabu kwa kuvunja sheria na miiko ya kijadi zilikuwa kali, lakini zililenga
zaidi kurekebisha, kurudisha na kudumisha amani ndani ya jamii.
Lugha na mawasiliano: Jamii za Kitanzania zilikuwa na aina nyingi za lugha za asili,
ambazo kwa kiasi kikubwa zilitokana na makabila ya jamii iliyohusika. Mathalani,
lugha za asili zilikuwa sehemu muhimu ya utambulisho wa jamii moja na nyingine
na zilitumika kuwasilisha maarifa, maadili na utamaduni kutoka kizazi kimoja
hadi kingine. Kwa mfano, methali, hadithi na nyimbo za jadi zilikuwa na jukumu
kubwa katika kufundisha maadili ya kijamii na kurithisha maarifa na historia. Pia,
mawasiliano ndani ya jamii yalifungamana sana na mila na desturi. Kwa mfano, jamii
ya Wachagga, walioishi kandokando na kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro,
walizungumza lugha ya Kichagga, ambayo ilitumika katika mawasiliano ya kila siku,
matambiko na desturi za kitamaduni, hivyo kubeba jukumu muhimu katika kudumisha
umoja na mshikamano katika jamii nzima.
Lugha katika jamii nyingi za Kitanzania ilikuwa na uhusiano wa karibu na mtindo
wa maisha yao pamoja na shughuli za uzalishaji mali kama vile kilimo na ufugaji.
Lugha ilitumika kama chombo cha kuhamasisha watu kushiriki katika shughuli
mbalimbali za uzalishaji mali. Kulikuwa na aina mbalimbali za ngoma kulingana
na jamii iliyohusika; kwa mfano, Wasukuma walikuwa na ngoma ya Bugobogobo,
Wanyasa walikuwa na ngoma ya Mganda, Wamakonde walikuwa na ngoma ya
Sindimba na Wazaramo pamoja na Waluguru walikuwa na ngoma ya Mdundiko.
Ngoma hizi zilichezwa katika matukio muhimu ya kijamii kama vile harusi, msimu
wa mavuno, au kuashiria kuanza kwa msimu wa kilimo. Muhimu zaidi, ngoma hizi
zilikuwa ni zao la lugha na zilitumika pia kama njia ya mawasiliano. Kupitia ngoma
27
03/10/2024 18:15:10
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 27 03/10/2024 18:15:10
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 27

