Page 33 - Historia_Maadili
P. 33

Zoezi la       2.1


           1.  Bainisha misingi mikuu ya maadili ya jamii za Kitanzania wakati ukoloni
               unaingia.

           2.  Eleza  umuhimu  wa kujifunza  maadili  ya  jamii  za  Kitanzania  ya  wakati
        FOR ONLINE READING ONLY
               uliopita.
           3.  Linganisha mfumo wa maadili wa jamii za Kitanzania kabla na baada ya
               ukoloni.


          Hali ya maadili ya jamii za Kitanzania wakati ukoloni unaingia imejipambanua katika
          nyanja mbalimbali ikijumuisha vipengele mbalimbali.

          Mila na desturi: Wakati wa kuingia kwa ukoloni, jamii za Kitanzania zilikuwa
          na mifumo thabiti ya maadili iliyoongozwa na kanuni, miiko, mila na desturi zao.
          Maadili kama vile uvumilivu, ukarimu, heshima kwa wazee na mamlaka, uadilifu,
          kujitolea, usawa na uwajibikaji yalikuwa sehemu muhimu ya maisha ya kila siku.
          Kila jamii ilikuwa na taratibu zake za kimaadili ambazo zilisimamiwa na viongozi
          wa jadi pamoja na wazee wa ukoo.

          Vilevile, jamii za Kitanzania zilikuwa na utajiri mkubwa wa mila, desturi, kanuni,
          miiko na utaratibu uliorithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Kwa mfano, kundi
          la wazee wa ukoo liliheshimiwa sana na lilitegemewa katika kufanya uamuzi, ushauri,
          kupitisha ujuzi wa kitamaduni na kudumisha umoja wa familia. Wazee walikuwa na
          wajibu wa kurithisha mila na desturi kwa kizazi kijacho. Walitumia njia mbalimbali
          kama vile masimulizi, nyimbo, ushairi, uelimishaji, malezi, ngoma na mbinu nyingine
          zilizolenga kuyalinda na kuyakuza maadili ya jamii iliyohusika.

          Pia, jamii zilijikita katika maisha ya jumuiya na uwajibikaji wa pamoja, ambapo
          imani ilikuwa ni suala la jamii nzima na si la mtu mmoja mmoja. Ustawi wa jamii
          haukuangalia masilahi ya mtu binafsi, bali uliangazia maadili ya kijamii kama vile
          ushirikiano na msaada wa pande zote, ambayo yalikuwa msingi wa maisha ya jamii.
          Shughuli za uzalishaji mali kama kilimo, uvuvi, uwindaji na uchungaji wa mifugo
          zilifanywa kwa pamoja katika jamii nyingi. Aidha, kulikuwa na mgawanyo wa
          majukumu kati ya wanaume na wanawake, ambapo wanaume walikuwa na jukumu
          la kutunza familia na wanawake walishiriki katika malezi ya watoto, kazi za nyumbani
          na wakati mwingine kilimo au shughuli nyingine za kiuchumi. Malezi ya watoto
          yalikuwa ni jukumu la jamii nzima.

          Maadili haya yaliimarishwa kupitia matambiko, sherehe na shughuli za kila siku.
          Vilevile, maadili yalisisitiza umuhimu wa kudumisha maelewano, ushirikiano na
          mshikamano wa kijamii. Hii iliwawezesha Watanzania kuendeleza mila na desturi
          zao kwa njia za vitendo na kujijenga kwenye misingi ya maisha yao.

                                                  25




                                                                                        03/10/2024   18:15:09
   HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd   25
   HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd   25                                         03/10/2024   18:15:09
   28   29   30   31   32   33   34   35   36   37   38