Page 28 - Historia_Maadili
P. 28
ambapo kulikuwa na hospitali maalumu kwa Wazungu na nyingine kwa ajili ya watu
wenye rangi nyingine. Kwa mfano, Hospitali ya Ocean Road ilikuwa maalumu kwa
Wazungu, kwa kuwa ilitoa huduma bora zaidi.
Miundombinu: Katika kutekeleza mpango wa ukoloni wa kupata malighafi muhimu
kwa ajili ya viwanda vya Ulaya, Waingereza waliendelea kufufua na kuanzisha
FOR ONLINE READING ONLY
miundombinu kutoka maeneo ya pwani hadi maeneo ya uzalishaji mali kama migodi
na mashamba ya pamba, mkonge na kahawa. Miundombinu iliyojengwa ni pamoja
na barabara, reli na bandari. Reli kutoka Tabora hadi Mwanza ilikamilishwa mwaka
1928. Pia, usafiri katika Ziwa Tanganyika na Viktoria uliimarishwa. Bandari za Tanga
na Dar es Salaam, ambazo zilikuwa zimeathiriwa na vita, zilikarabatiwa. Waingereza
pia walijenga bandari ya Mtwara. Aidha, miundombinu mingine ya reli iliongezwa
kwa lengo la kusafirisha malighafi na vibarua kutoka sehemu mbalimbali za nchi,
kama inavyoonekana kwenye Kielelezo 1.5.
Kielelezo 1.5: Miundombinu ya reli wakati wa utawala wa Waingereza
Miundombinu ya barabara, reli na usafiri wa majini ililenga kuunganisha maeneo
muhimu ya uzalishaji mali, kama vile mashamba ya mkonge, pamba, karanga na
20
03/10/2024 18:15:09
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 20
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 20 03/10/2024 18:15:09

