Page 23 - Historia_Maadili
P. 23
Zoezi la 1.4
1. Fafanua namna mabadiliko katika mfumo wa utawala wa jadi kufuatia kuja
kwa Wajerumani yalivyoathiri jamii za Kitanzania.
2. Kwa nini jamii za Kitanzania zilipinga ulipaji wa kodi ulioanzishwa na
FOR ONLINE READING ONLY
utawala wa Kijerumani?
3. Unajifunza nini kutoka kwa mababu na mabibi zetu waliopinga mfumo na
utawala wa Kijerumani?
Utawala wa Waingereza Tanganyika na Zanzibar
Afrika Mashariki ya Kijerumani ilikuwa sehemu ya koloni la Ujerumani hadi
kumalizika kwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia mwaka 1918. Wakati wa vita hivyo,
koloni la hili lilitekwa na majeshi ya Uingereza na Ubelgiji. Mkataba wa Amani
wa Versailles wa mwaka 1919 uliamua kwamba makoloni yote yaliyokuwa ya
Wajerumani yakabidhiwe mataifa yaliyoshinda vita hivyo. Hivyo, Afrika Mashariki
ya Kijerumani ilikabidhiwa rasmi kwa Waingereza chini ya udhamini wa Jumuiya
ya Kimataifa (League of Nations).
Kwa upande wa Zanzibar, utawala wa Waingereza ulianza baada ya kutiwa saini kwa
mkataba wa pili kati ya Wajerumani na Waingereza. Mkataba huo ulisainiwa tarehe
1 Julai, 1890, unaojulikana kama Mkataba wa Heligoland. Kulingana na mkataba
huo, Uingereza ilipewa mamlaka ya kuiweka Zanzibar chini ya himaya yake kwa
makubaliano na mtawala wa wakati huo, Sayyid Ali bin Said.
Jamii za Tanganyika na Zanzibar wakati huo zilifuata mwelekeo wa kiuchumi,
kisiasa na kijamii ulioanzishwa na Waingereza. Ili kuimarisha ukoloni, Waingereza
walibadilisha mfumo wa utawala uliokuwapo na kuanzisha mfumo wa kiuwakala
ambao ulibadilisha pia uchumi, siasa na utamaduni wa Tanganyika. Jambo muhimu
la kufahamu ni kwamba, ni utawala wa Kiingereza uliobadilisha jina la koloni hilo
kutoka Afrika Mashariki ya Kijerumani na kuwa Tanganyika.
Mabadiliko ya kiuchumi wakati wa utawala wa Waingereza
Mabadiliko ya kiuchumi wakati wa utawala wa Waingereza yalilenga kuendeleza
kilimo, biashara na viwanda vidogovidogo. Kwa upande wa kilimo, utawala wa
Waingereza ulihamasisha kilimo cha mazao ya biashara kama vile kahawa, pamba,
mkonge, chai na pareto. Serikali hiyo pia iliwahimiza walowezi kufufua mazao ya
biashara ambayo yalikuwa yameathiriwa na vita. Walowezi hawa walitoka mataifa
mbalimbali kama Uingereza, Afrika Kusini, Ugiriki na India. Lengo kubwa la kufufua
mazao haya ya biashara lilikuwa kupata malighafi za kutosha kwa ajili ya viwanda
nchini kwao Uingereza.
15
03/10/2024 18:15:08
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 15
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 15 03/10/2024 18:15:08

