Page 18 - Historia_Maadili
P. 18
ya Kiarabu, huku lugha ya Kiswahili ikiendelea kutumika kama lugha ya biashara
na mawasiliano ya kila siku.
Mwingiliano baina ya Waarabu na jamii za pwani ulisababisha mabadiliko makubwa
ya kitamaduni. Kwa mfano, uvaaji wa mavazi kama vile kanzu, baibui, baraghashia na
makubadhi ulienea sana. Lugha ya Kiswahili pia ilianza kupata maneno mapya baada
FOR ONLINE READING ONLY
ya kutohoa baadhi ya msamiati kutoka lugha ya Kiarabu ili kurahisisha mawasiliano.
Mfano wa baadhi ya maneno hayo ni kama vile marhaba, shukrani, sheria, heshima,
nzuri, labeka na hayati. Jamii zilizoathiriwa zaidi na tamaduni za Kiarabu ni pamoja na
Wahadimu, Watumbatu, Wapemba,Wazaramo na Wakwere kutokana na mwingiliano
wao wa karibu katika shughuli za kila siku.
Kazi ya kufanya 1.3
Soma matini mbalimbali katika vitabu na mtandao kuhusu mabadiliko ya kijamii
wakati wa utawala wa Waarabu kisha; tengeneza vibonzo vinavyoonyesha namna
utamaduni, maadili na elimu vilivyobadilika baada ya ujio wa Waarabu.
Utawala wa Wajerumani
Utawala wa Wajerumani katika Afrika Mashariki ya Kijerumani ulisukumwa na
mabadiliko ya kiuchumi yaliyokuwa yakijitokeza barani Ulaya, ikiwemo nchini
Ujerumani. Mabadiliko hayo yalitokana na kuongezeka kwa teknolojia iliyochochea
mapinduzi ya viwanda yaliyoshika kasi kuanzia mwaka 1750 nchini Uingereza.
Mapinduzi hayo yalisababisha uzalishaji mkubwa wa bidhaa na hivyo kuongeza
mahitaji ya malighafi kwa ajili ya uzalishaji pamoja na masoko mapya na makubwa
kwa ajili ya kuuza bidhaa hizo. Ili kukabiliana na changamoto hii, Wajerumani, pamoja
na mataifa mengine ya Ulaya, walitafuta njia za kupata suluhisho kupitia nchi za nje.
Bara la Afrika lilionekana kuwa eneo muafaka kwa uwekezaji na utatuzi wa
changamoto za upatikanaji wa malighafi na masoko. Katika robo ya mwisho ya
karne ya 19, Wajerumani walifika Afrika Mashariki ya Kijerumani baada ya kupata
taarifa kuhusu uwapo wa malighafi na soko la bidhaa. Taarifa hizo walizipata kutoka
kwa wamisionari, wafanyabiashara na wapelelezi waliotumwa na makampuni ya
Kijerumani hapa nchini. Hii iliwasaidia sana kuyatambua maeneo muhimu ya
kuwekeza na kuanzisha mashamba makubwa ili kupata malighafi mbalimbali
zilizohitajika katika viwanda vya Ujerumani.
Utawala wa Wajerumani katika eneo hili unaweza kugawanywa katika vipindi
vifuatavyo: Kati ya mwaka 1886 hadi 1891. Kipindi hiki, Afrika Mashariki ya
Kijerumani ilitawaliwa na Kampuni ya Kijerumani ya Afrika Mashariki chini ya
uongozi wa mfanyabiashara Karl Peters. Kuanzia mwaka 1891 hadi 1918, serikali ya
10
03/10/2024 18:15:07
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 10
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 10 03/10/2024 18:15:07

