Page 15 - Historia_Maadili
P. 15

wakulima wadogo wadogo, raia wa kawaida, huku tabaka la tatu likiwa la watwana
          na watumwa. Kuja kwa Waarabu kulibadilisha mfumo wa utawala wa kidemokrasia
          ya kijadi na umoja uliokuwa ukiendeshwa na tawala za kijadi. Mfumo huu mpya
          ulileta mgawanyiko katika jamii. Mfano wa mgawanyiko huo ni jamii za Kizanzibari
          zilipoteza mifumo yao ya kiuongozi ya kijadi na badala yake, mfumo wa kiutawala
          wa Kiarabu kushika hatamu visiwani humo. Hivyo, Waarabu walisababisha migogoro
        FOR ONLINE READING ONLY
          katika jamii za pwani ya Tanganyika na Zanzibar.

          Miongoni mwa mbinu walizozitumia na Waarabu ni kuwagawa watawala wa jadi
          kwa kumuunga mkono mtawala aliyeonekana kuwa na nguvu zaidi kuliko wenzake
          na wale walioonekana kuwa wasaliti. Kwa upande wa Zanzibar, watawala wa jadi
          kama Mwinyi Mkuu alifanywa kuwa mshirika mwenza katika utawala. Waarabu
          walitumia uongozi wa mabavu, unyanyasaji na ukandamizaji kwa wananchi. Kwa
          mfano, wananchi walifanyishwa kazi ngumu bila malipo, walinyang’anywa ardhi
          yenye rutuba na Waafrika wengi walichukuliwa na kupelekwa sehemu zingine kama
          watumwa.


           Kazi ya kufanya 1.2

            Soma vitabu na matini mbalimbali kwenye mtandao, kisha fanya uchunguzi
            katika mfumo wa umiliki wa ardhi kabla na baada ya ujio wa Waarabu visiwani
            Zanzibar na Pemba. Uchunguzi wako ujikite katika maeneo yafuatayo:
             (a)  Namna mfumo wa umiliki wa ardhi ulivyokuwa kabla ya ujio wa utawala
                  wa Waarabu;
             (b)  Mabadiliko  yaliyoletwa  na utawala  wa  Waarabu katika  mfumo wa
                  umiliki wa ardhi; na
             (c)  Athari zilizoletwa na mabadiliko katika mfumo wa umiliki wa ardhi.



          Mabadiliko ya kiuchumi wakati wa utawala wa Waarabu
          Kuongezeka kwa mahitaji ya pembe za ndovu, karafuu, mafuta ya nazi na mpira
          katika viwanda vya Ulaya na Marekani kulimhamasisha sana Sultani wa Zanzibar
          pamoja na wafanyabiashara wa Kiarabu kuendeleza biashara ya bidhaa hizo. Hali
          kadhalika, mashamba makubwa ya mikarafuu na mpira yalianzishwa visiwani, jambo
          lililosababisha ongezeko la mahitaji ya nguvukazi hasa vibarua wa kupalilia, kuchuma
          karafuu na kuangua nazi.

          Waarabu walifanya biashara na wenyeji wa pwani ya Tanganyika na Afrika Mashariki
          kwa ujumla. Katika biashara hiyo, walitafuta dhahabu, shaba, pembe za ndovu,
          magogo ya mikoko, nta na ngozi za wanyama pori kama vile chui na pundamilia.
          Vingine ni magamba ya konokono na kobe, pamoja na watumwa. Waarabu nao
          walileta bidhaa mbalimbali kama manukato, vyombo vya nyumbani, viungo vya


                                                  7




                                                                                        03/10/2024   18:15:07
   HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd   7
   HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd   7                                          03/10/2024   18:15:07
   10   11   12   13   14   15   16   17   18   19   20