Page 16 - Historia_Maadili
P. 16

chakula kama vile karafuu, mdalasini na tangawizi. Bidhaa nyingine zilikuwa shanga,
          majambia, bunduki, vioo vya kujitazamia na nguo. Kutokana na ustawi wa biashara
          hiyo, Zanzibar iliimarika na kuwa dola kuu ya kibiashara katika eneo la Afrika
          Mashariki likijumuisha pwani wa Bahari ya Hindi, mashariki mwa Kongo, Malawi
          and kaskazini mwa Msumbiji.

        FOR ONLINE READING ONLY
          Biashara za masafa marefu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati zilifanyika
          kwa kutumia njia kuu tatu zilizoanzia pwani kuelekea bara, kama inavyooneshwa
          kwenye Kielelezo 1.4. Njia ya Kaskazini ilianzia Saadani kuelekea Pangani hadi
          Mlima Kilimanjaro, kisha kuingia nchini Kenya. Njia ya kati ilianzia Bagamoyo kupitia
          Morogoro hadi Tabora. Ilipofika Tabora, iligawanyika katika matawi mawili: tawi la
          kwanza lilianzia Tabora kuelekea  kaskazini huko Karagwe, Buganda na Bunyoro. Tawi
          la pili lilianzia Tabora kuelekea magharibi huko Ujiji, Burundi, Rwanda, Katanga na
          Umanyema huko Kongo. Njia hii ilimilikiwa zaidi na Wanyamwezi na Wasumbwa.


















































               Kielelezo 1.4: Njia kuu za biashara ya masafa marefu wakati wa utawala wa Waarabu


                                                  8




                                                                                        03/10/2024   18:15:07
   HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd   8                                          03/10/2024   18:15:07
   HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd   8
   11   12   13   14   15   16   17   18   19   20   21