Page 12 - Historia_Maadili
P. 12
Waingereza walitawala Tanganyika kuanzia mwaka 1919 hadi 1961. Baada ya Vita
Kuu ya Kwanza ya Dunia, Tanganyika iliwekwa chini ya udhamini wa Jumuiya ya
Mataifa (League of Nations) na baada ya Vita Kuu ya
Pili ya Dunia, chini ya Umoja wa Mataifa (United
Nations Organisation). Hata hivyo, taasisi hizo ziliipa
Uingereza mamlaka ya kuitawala Tanganyika na
FOR ONLINE READING ONLY
kuiandaa kujitawala yenyewe. Hivyo, kuanzia mwaka
1919, Tanganyika ilikuwa chini ya utawala wa
Waingereza, ambapo Sir Horace Byatt alikuwa Gavana
wa kwanza. Kielelezo 1.1 kinaonesha picha ya Gavana
Sir Horace Byatt. Kielelezo 1.1: Gavana Sir
Horace Byatt
Kuanzia mwaka 1919 hadi 1925, Waingereza waliendeleza muundo wa utawala
waliourithi kutoka kwa Wajerumani. Hata hivyo, kuanzia mwaka 1926, chini ya
uongozi wa Gavana Sir Donald Cameron, Waingereza walibadilisha mfumo huo
na kuanzisha utawala wa kiuwakala. Katika mfumo huu mpya, walitumia mamlaka
za jadi kutekeleza sera za kikoloni. Tofauti na utawala wa Wajerumani, mfumo
huu haukuwa na ukatili mkubwa. Mifumo na utawala wa Waarabu, Wajerumani na
Waingereza imefafanuliwa kwa kina katika sehemu zinazofuata.
Zoezi la 1.1
1. Kwa nini Waingereza walibadilisha mfumo wa utawala kutoka utawala wa
moja kwa moja hadi mfumo wa uwakala?
2. Eleza jinsi mifumo ya utawala wa Waarabu, Wajerumani na Waingereza
ilivyoyaathiri maendeleo ya jamii za Kitanzania.
3. Tofautisha mifumo ya utawala wa Waarabu, Wajerumani na Waingereza
katika Tanzania.
Utawala wa Waarabu
Waarabu kutoka Oman walifika Zanzibar na Tanganyika mwishoni mwa karne ya
18. Kwa madhumuni ya kutawala, walijenga makazi yao katika maeneo ya Unguja,
Pemba na pwani ya Tanganyika, hususani katika miji ya Kilwa, Tanga na Bagamoyo,
kama inavyoonyeshwa kwenye Kielelezo 1.2.
4
03/10/2024 18:15:06
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 4 03/10/2024 18:15:06
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 4

