Page 8 - Historia_Maadili
P. 8
Dibaji
Kitabu hiki cha Historia ya Tanzania na Maadili, Shule za Sekondari kimeandikwa
FOR ONLINE READING ONLY
mahususi kwa ajili ya mwanafunzi wa Kidato cha Pili katika Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania. Kitabu hiki kimeandaliwa kulingana na Muhtasari wa Somo la Historia
ya Tanzania na Maadili uliotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wa
mwaka 2023.
Kitabu hiki kina sura sita: Ukoloni katika jamii za Kitanzania, Athari za ukoloni
katika maadili ya Kitanzania, Mapambano ya awali dhidi ya uvamizi wa kikoloni,
Harakati za kudai uhuru wa Tanganyika na Zanzibar, Ujenzi wa Taifa baada ya ukoloni
na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Maudhui ya kitabu hiki yamewasilishwa kwa
njia ya matini, kazi za kufanya, vielelezo, pamoja na picha zinazochochea ujenzi wa
umahiri unaokusudiwa kwa kila sura. Vilevile, katika kila sura kuna mazoezi yenye
lengo la kupima na kujenga uelewa pamoja na ujuzi katika somo hili. Hivyo, unapaswa
kufanya mazoezi na kazi zote zilizopo kwenye kitabu hiki, pamoja na kazi nyingine
utakazopewa na mwalimu.
Jifunze zaidi kupitia maktaba mtandao https://ol.tie.go.tz au ol.tie.go.tz
Taasisi ya Elimu Tanzania
viii
03/10/2024 18:15:05
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 8
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 8 03/10/2024 18:15:05

