Page 9 - Historia_Maadili
P. 9
Sura ya Kwanza Ukoloni katika jamii
za Kitanzania
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Kipindi ukoloni unaingia, jamii nyingi za Kitanzania zilikuwa zimepiga hatua
katika maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Katika sura hii, utajifunza
kuhusu chimbuko, ukuaji, mifumo na mchango wa ukoloni katika uhusiano
wa Tanzania na mataifa yaliyoitawala. Umahiri utakaoujenga utakuwezesha
kuthamini maendeleo ya jamii za Kitanzania katika kipindi cha ukoloni. Pia,
utaweza kushiriki vyema katika juhudi za kuleta maendeleo ya Tanzania.
Fikiri
Hali ya jamii za Kitanzania wakati ukoloni unaingia.
Chimbuko na ukuaji wa ukoloni
Ukoloni ni hali ya nchi moja huitawala nchi nyingine katika nyanja zote za kiuchumi,
kisiasa na kiutamaduni. Katika muktadha huu, uchumi, siasa na utamaduni wa nchi
zinazotawaliwa hutumiwa kwa malengo ya wakoloni. Ukoloni ulitokana na kustawi
kwa mfumo wa ubepari, ambao ulifikia hatua ya ubeberu huko Ulaya Magharibi.
Ubeberu huu uliwalazimu wakoloni kuvuka mipaka ya nchi zao ili kutafuta rasilimali
na masoko mapya ya bidhaa zao na sehemu za kuwekeza mitaji.
Ukuaji wa ubepari katika robo ya mwisho ya karne ya 19 uliambatana na mapinduzi na
maendeleo ya viwanda katika nchi za Ulaya Magharibi. Maendeleo hayo ya viwanda
yalisababisha ongezeko kubwa la mahitaji ya malighafi hasa za kilimo na madini
kwa ajili ya uzalishaji viwandani. Katika kipindi hicho, malighafi kutoka makoloni
mengine kama vile Australia, Kanada na Bara la Asia hasa India ya Uingereza (British
India) hazikutosheleza mahitaji ya viwanda. Baada ya nchi za Ulaya Magharibi
kutuma wapelelezi miaka ya 1850 hadi 1870 waligundua kuwa Bara la Afrika lina
uwezo wa kuzalisha malighafi za kutosha kwa ajili ya viwanda vya Ulaya Magharibi.
Mataifa kama Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Ubelgiji na Ureno yalivutiwa na
rasilimali hasa ardhi yenye rutuba, misitu, mito, wanyama pori na madini barani
Afrika.
1
03/10/2024 18:15:05
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 1 03/10/2024 18:15:05
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 1

