Page 13 - Historia_Maadili
P. 13
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo 1.2: Maeneo ambayo Waarabu waliweka ngome za utawala wao
Watawala wa Kiarabu waliotawala pwani ya Afrika Mashariki walifika nchini katika
vipindi mbalimbali. Wengi wao walivutiwa na utajiri wa rasilimali uliokuwapo katika
eneo hili. Utajiri huo ulijulikana kutokana na uhusiano wa kibiashara wa muda mrefu
kati ya pwani ya Afrika Mashariki na nchi za bara la Asia kama vile Omani, Uhindi,
Uchina na Uajemi.
Mtawala wa kwanza wa Kiarabu katika eneo hili alijulikana kama Sultani Seyyid Said
bin Sultan. Sultani huyu alikuwa Mwarabu wa kwanza kutawala kwa pamoja dola za
Omani na Zanzibar, kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1800 hadi alipofariki dunia
mwaka 1856. Sultani alivutiwa sana na hali ya hewa ya Zanzibar, pamoja na kustawi
kwa biashara katika ukanda huo, kina kirefu cha bandari ya Zanzibar na udongo
wenye rutuba uliostawisha mazao mbalimbali, kama vile mikarafuu na minazi. Hivyo,
kiongozi huyu aliwahimiza matajiri wa Kiarabu kutoka Omani kuhamia Zanzibar na
kuanzisha mashamba makubwa ya mikarafuu. Mnamo mwaka 1840, Sultani Seyyid
Said alihamisha rasmi makao yake kutoka Muscat, Omani hadi Zanzibar na kuifanya
5
03/10/2024 18:15:06
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 5
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 5 03/10/2024 18:15:06

