Page 14 - Historia_Maadili
P. 14
Zanzibar kuwa makao makuu ya utawala wake. Baada ya kifo chake mwaka 1856,
urithi wa utawala ulifuata kwa watawala wengine, akiwemo Sultani Seyyid Majid,
Sultani Barghash na hatimaye Sultani Jamshid bin Abdullah Al Said. Jamshid bin
Abdullah Al Said alizaliwa tarehe 16 Septemba 1929 na kuwa Sultan wa Zanzibar
baada ya kifo cha baba yake, Abdullah Bin Khalifa mwezi Julai 1963. Yeye alikuwa
Sultan wa mwisho wa Zanzibar kutoka kwa familia ya al Busaid wa Oman waliotawala
FOR ONLINE READING ONLY
kwa miaka 91.
Mabadiliko ya kisiasa wakati wa utawala wa Waarabu
Jamii za pwani ya Tanganyika na Zanzibar zilikuwa na mfumo madhubuti wa uongozi,
utoaji wa uamuzi na umiliki wa ardhi kabla ya kuja kwa Waarabu wa Oman. Hivyo,
ardhi katika jamii nyingi ilimilikiwa kwa pamoja na jamii nzima. Kila mwanajamii
alikuwa na uhuru wa kuchagua sehemu za kulima, kukata miti au kufuga. Ardhi
ambayo haikutumiwa kwa wakati huo ilikuwa ikihifadhiwa kwa matumizi ya baadaye
ya jamii nzima. Hata hivyo, baada ya kuja kwa Waarabu, mabadiliko yalitokea. Kwa
mfano, Waarabu walianzisha mtindo mpya wa kilimo cha mazao ya biashara, ambao
ulisababisha baadhi ya jamii za pwani ya Tanganyika na Zanzibar kuporwa ardhi yao
yenye rutuba na kugawiwa kwa wakulima wa mazao ya biashara wa Kiarabu.
Kama ilivyokuwa kwa wakoloni wengine, Waarabu walitekeleza sera za kuchukua
sehemu kubwa ya ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo cha mikarafuu na minazi.
Ili kufanikisha mpango huo, Sultani Seyyid Said alihamasisha kwa kiasi kikubwa
kilimo cha mikarafuu na minazi. Sehemu kubwa ya ardhi ya Zanzibar, ambayo awali
ilitumiwa kwa kilimo cha mazao ya chakula,
ilichukuliwa na mamwinyi wa Kiarabu na
kuanzishwa mashamba makubwa ya
mikarafuu na minazi. Mfumo huu mpya wa
uongozi na siasa kwa ujumla, ulioruhusu
ardhi yenye rutuba kumilikiwa na Waarabu,
uliwafanya wananchi kuwa watumwa katika
nchi yao. Katika mazingira haya, heshima,
uwezo, haki na mali za Wazanzibari
zilinyakuliwa na utawala wa Sultani.
Kielelezo 1.3 kinaonesha picha ya Sultani
Seyyid Said. Kielelezo 1.3: Sultani Seyyid Said
Mtindo mpya wa ugawaji ardhi uliathiri mfumo wa kisiasa wa jadi wa umiliki wa
ardhi kwa wanajamii wote, hali iliyosababisha kuibuka kwa matabaka katika jamii.
Tabaka la kwanza lilikuwa la wanyonyaji, likiongozwa na viongozi wa serikali,
wafanyabiashara wa kihindi na mamwinyi hasa wa Kiarabu. Tabaka la pili lilijumuisha
6
03/10/2024 18:15:06
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 6 03/10/2024 18:15:06
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 6

