Page 26 - Historia_Maadili
P. 26
Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Waingereza walipanua Baraza la Kutunga
Sheria. Baraza hili lilikuwa na kazi ya kumshauri Gavana kuhusu masuala mbalimbali
yanayohusu utawala. Jukumu jingine la baraza lilikuwa ni kutunga sheria ambazo
zilihitaji idhini kutoka serikali ya Uingereza kabla ya kutumika. Wajumbe wa Baraza
la Kutunga Sheria waliingia kwa kuteuliwa na Gavana mwenyewe, huku wengine
wakiteuliwa kutokana na nyadhifa zao serikalini. Baraza hili kwa mara ya kwanza
FOR ONLINE READING ONLY
lilijumuisha machifu wa Kitanganyika, wakiwemo Chifu Abdieli Shangali na Chifu
Kidaha Makwaia.
Zanzibar ilikuwa na uhusiano maalumu na Waingereza, lakini kwa hali halisi, siasa
ya Waingereza iliifanya Zanzibar kuwa koloni. Ingawa Waingereza waliutumia
utawala wa Sultani katika kuitawala Zanzibar, utawala wa Kisultani haukujitegemea
hata mara moja. Mwanzoni mwa mwaka 1914, Baraza la Ushauri lilianzishwa kwa
lengo la kumshauri Sultani na serikali yake kuhusu masuala ya serikali. Unguja na
Pemba ziligawanywa katika wilaya, mudiria na shehia. Kila wilaya ilikuwa chini
ya afisa wa serikali ambaye alikuwa Mwingereza, huku Mudir na Sheha wa Kiarabu
wakisimamia mudiria na shehia. Hata hivyo, kulikuwa na Waafrika wachache
waliokuwa wakisimamia shehia, lakini walipewa jukumu la kuwahimiza wenzao
kuwatumikia Wazungu, Waarabu na Wahindi.
Zoezi la 1.5
1. Tofautisha mfumo wa utawala wa Waingereza na ule wa Wajerumani katika
kuzitawala jamii za Kitanzania.
2. Eleza kwa kifupi majukumu ya viongozi wa jadi katika serikali ya Kiingereza.
3. Linganisha majukumu ya viongozi wa sasa wa serikali za mitaa na yale ya
viongozi wa jadi wakati wa utawala wa Waingereza Tanganyika.
4. Tofautisha utawala wa Waingereza Tanganyika na Zanzibar.
Mabadiliko ya kijamii wakati wa utawala wa Waingereza
Mabadiliko ya kijamii wakati wa utawala wa Waingereza yalijikita zaidi katika utoaji
wa huduma za msingi kama elimu, afya, maji, umeme na miundombinu. Huduma
hizi zilitolewa kwa madhumuni ya kuiwezesha serikali ya Waingereza kurahisisha
utekelezaji wa malengo ya kikoloni, ikiwemo kupata nguvukazi ya kutosha miongoni
mwa wananchi ili kuwezesha uzalishaji wa malighafi muhimu kwa viwanda vyao huko
Ulaya. Kwa kiasi kikubwa, huduma za jamii zilizoanzishwa na serikali ya kikoloni
hazikulenga kuwahudumia wananchi bali kutimiza masilahi ya wakoloni.
Elimu: Shughuli za utoaji wa elimu ziliathirika sana wakati wa Vita Kuu ya Kwanza
ya Dunia. Serikali ya Uingereza, kwa kushirikiana na mashirika ya dini, ilianza
kutoa elimu kwa wananchi kwa kufuata mipango na mahitaji ya wakoloni. Sehemu
18
03/10/2024 18:15:08
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 18 03/10/2024 18:15:08
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 18

