Page 38 - Historia_Maadili
P. 38

maarufu. Hata hivyo, mavazi ya kitamaduni yaliendelea kutumika, hasa katika maeneo
          ya vijijini na miongoni mwa wale waliopinga ushawishi wa wakoloni na tamaduni
          za Ulaya Magharibi.

          Aidha, maadili ya Kitanzania wakati wa kuingia kwa ukoloni yalikuwa na nguvu
          kubwa katika maisha ya watu na yalidumishwa kwa umakini na viongozi wa jadi
        FOR ONLINE READING ONLY
          pamoja na wazee wa mila. Kanuni hizi za kimaadili zilifanya kazi kama misingi
          imara iliyojenga jamii. Jamii pia ilionesha uwajibikaji mkubwa katika kutekeleza
          wajibu wao kwa familia na jamii kwa ujumla. Maadili haya yaliziwezesha jamii za
          Kitanzania kujiendeleza na kusaidia kuunda jamii zenye utulivu, mshikamano na
          maendeleo endelevu.


           Kazi ya kufanya 2.3


            Tafuta taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo mtandao na eleza jinsi mavazi
            yanaweza kutumika katika kudumisha maadili ya Kitanzania.




                              Zoezi la          2.2


            1.  Ainisha maadili yanayopaswa kudumishwa katika jamii yako.
            2.  Pendekeza mikakati ya kudumisha maadili katika jamii yako.

            3.  Eleza jinsi teknolojia inavyoathiri maadili katika jamii unayoishi.

            4.  Ni kwa namna  gani  hadithi  na masimulizi  yanaweza  kutumika  katika
               kujenga uzalendo katika mazingira ya sasa.

            5.  Eleza umuhimu wa lugha za asili katika kudumisha maadili katika mazingira
               ya sasa.




          Athari za mfumo wa ukoloni katika maadili ya Kitanzania
          Kuingia kwa mfumo wa kikoloni katika jamii za Kitanzania kuliathiri mifumo ya
          maadili ya kijamii, kiutamaduni, kisiasa na kiuchumi. Athari hizi zinaelezwa kwa
          upana katika sehemu zinazofuata.



          Athari za kijamii
          Elimu: Kabla ya ukoloni, elimu katika jamii za Kitanzania ilitolewa kulingana na

          mazingira yao na ilijikita katika mila na desturi. Kulikuwa na mfumo rasmi wa

                                                  30




                                                                                        03/10/2024   18:15:10
   HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd   30
   HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd   30                                         03/10/2024   18:15:10
   33   34   35   36   37   38   39   40   41   42   43