Page 36 - Historia_Maadili
P. 36
hizo, wanajamii waliweza kujenga uzalendo, ujasiri, upendo, fahari na mshikamano
wa kijamii.
Simulizi na hadithi: Simulizi na hadithi zilikuwa nguzo muhimu za mawasiliano
katika jamii za Kitanzania. Kila jamii ilikuwa na aina zake za masimulizi yaliyoakisi
tamaduni zao. Baadhi ya masimulizi hayo ni kama vile hekaya, methali, vitendawili na
FOR ONLINE READING ONLY
hadithi, ambazo zilitumika kufundisha, kuendeleza na kurithisha maadili ya kitamaduni
kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Kwa mfano, hadithi zilikuwa na masimulizi ya
matukio mbalimbali ya kijamii yaliyotokea katika vipindi vya nyuma ndani ya jamii
husika. Hivyo, hadithi hizi ziliwafundisha, ziliwaburudisha na kuwaonya na kwa njia
hiyo ziliweza kusaidia katika ujenzi wa maadili ndani ya jamii. Mathalani, jamii ya
Wahehe ilitumia ushairi kama njia ya kuwasilisha ujumbe, kuwaelimisha vijana na
kuwaburudisha. Simulizi hizi zilikuwa muhimu sana katika kuudumisha utambulisho
wa kitamaduni na maadili ya kijamii. Wazee wa jamii walikuwa wahusika wakuu
katika utoaji wa simulizi na hadithi hizi.
Kazi ya kufanya 2.2
Tafuta taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo mitandao kuhusu lugha ya
kabila mojawapo la Tanzania. Kisha, bainisha misemo au methali au vitendawili
vya makabila hayo ambavyo vinalenga kudumisha maadili ya Kitanzania.
Mavazi: Wakati wa kuingia kwa ukoloni, jamii za Kitanzania zilikuwa na mavazi ya
asili yaliyotengenezwa kwa kutumia malighafi za kiasili kama vile ngozi za wanyama,
majani na magome ya miti. Vilevile, walivaa mapambo kama hereni na bangili.
Mavazi haya yalikuwa sehemu ya utambulisho na yaliheshimu utamaduni wa kabila
au jamii iliyohusika. Vitu hivyo vilikuwa zaidi ya mavazi kwani viliashiria umuhimu
wa utamaduni uliowakilisha, hadhi, umri na hali ya ndoa ndani ya jamii.
Vilevile, jamii za Wachaga wanaoishi kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro
walikuwa wakivaa mavazi yaliyotengenezwa kwa ngozi ya wanyama au vitambaa
vilivyofumwa kienyeji. Mavazi haya mara nyingi yalikuwa rahisi na yalifaa kwa hali
ya hewa ya mlima. Hata hivyo, baada ya kuwasili kwa ukoloni, mavazi ya mtindo
wa Kimagharibi yalianza kuathiri mavazi yao, hasa miongoni mwa vijana na wale
waliojihusisha na biashara au shughuli za kimisionari. Hii ilikuwa ni sehemu ya
harakati za wazungu kutafuta masoko kwa bidhaa za viwanda vyao vya Ulaya.
28
03/10/2024 18:15:10
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 28
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 28 03/10/2024 18:15:10

