Page 37 - Historia_Maadili
P. 37
Halikadhalika, miongoni mwa jamii ya Wasukuma, mavazi ya kitamaduni
yalitengenezwa kwa ngozi ya wanyama na nyuzi za mimea kabla ya kuanzishwa
kwa nguo za kufuma. Wanawake pia walivaa sketi za nyasi zilizotengenezwa kwa
nyuzi za mimea. Mavazi haya yalikuwa rahisi lakini yalilingana na mazingira na hali
ya hewa ya Usukumani. Aidha, nguo hizo ziliakisi shughuli za kilimo na ufugaji ya
jamii ya Wasukuma. Mavazi pia yaliendana na mitindo ya urembo mathalani mitindo
FOR ONLINE READING ONLY
ya kusuka nywele kwa wanawake na kunyoa nywele kwa wanaume kwa mfano kwa
jamii ya Wanyamwezi kama inavyoonekana katika Kielelezo 2.2. Kwa ushawishi
wa kikoloni, nguo za pamba zikawa za kawaida zaidi na mavazi ya jadi kama vile
kaniki yalianza kuhifadhiwa kwa matukio maalumu. Kielelezo 2.1 kinaonesha vazi
la asili la kaniki la jamii ya Wasukuma.
Kielelezo 2.1: Vazi la asili Kielelezo 2.2: Mitindo ya nywele katika
katika jamii ya Wasukuma jamii ya Wanyamwezi
Jamii za Wanyamwezi, Wasukuma, Wahehe, Wachaga, Wahaya na Wasambaa zilikuwa
na utofauti wa mavazi kati ya wananchi na watawala wao. Kulikuwa na nguo maalumu
zilizovaliwa na watawala ili kuonesha mamlaka yao. Mavazi hayo ni pamoja na nguo
za ngozi za wanyama hasa simba na chui, kofia, regalia, taji, mapambo na mkoba.
Mavazi haya yaliandamana na vifaa kama usinga, ngao na mkuki kama alama za
nguvu, mamlaka na utawala wa eneo la kiongozi. Pia, kulikuwa na nguo maalumu
zilizovaliwa na wazee walioongoza kufanya matambiko ya kijamii. Nguo hizi zilikuwa
na rangi maalumu. Nguo nyeupe na nyeusi ndio ziliruhusiwa kwa ajili ya matambiko.
Nguo nyekundu hazikuruhusiwa kutumika katika matambiko.
Mavazi na mitindo ya kikoloni iliingia na kuenea katika jamii za Kitanzania.
Wamisionari, maofisa wa kikoloni na wafanyabiashara walileta aina mpya za nguo
kama vile suruali, mashati, gauni na suti. Vilevile, katika maeneo ya pwani na vituo
vya kibiashara kama Ujiji na Tabora, ambako biashara zilifanyika kati ya jamii za
Kitanzania na Waarabu, mavazi kama kanzu, baibui, makubadhi na vikoi yalikuwa
29
03/10/2024 18:15:10
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 29 03/10/2024 18:15:10
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 29

