Page 41 - Historia_Maadili
P. 41
mkubwa ikienea maeneo mengi nchini na idadi ya waumini ikaongezeka. Waumini
wapya walionekana kujitolea kwa imani yao, wakichukua nafasi za uongozi katika
jamii na kusaidia kuendeleza mafundisho mapya.
Mbali na Watanzania wengi kuingia kwenye dini ya Kikristo, mabadiliko ya dini
yalisababisha pia mabadiliko katika maadili na taratibu za Kitanzania, kama vile
FOR ONLINE READING ONLY
masuala ya ndoa, tohara, mavazi, vyakula na muziki. Desturi na mila za Kitanzania
zilipuuzwa na badala yake, desturi na mila za kigeni zikapewa umuhimu mkubwa.
Hii ilisababisha mkanganyiko katika kulea watoto kati ya utamaduni wa Kitanzania
na mafundisho ya Kikristo.
Muingiliano na uhusiano wa dini na ukoloni pia ulisababisha mgawanyiko katika
jamii ya Kitanzania. Baadhi ya watu waliokubaliana na utamaduni wa kikoloni
walionekana kama wasaliti wa imani na maadili ya Kitanzania. Vilevile, kulikuwa na
wale waliopinga mabadiliko haya ya kikoloni, wakidai kwamba utamaduni na hasa
imani za asili, zinahitaji kulindwa na kuheshimiwa. Hivyo, kukandamizwa kwa dini
za jadi kulichangia kuzizorotesha, kwani vizazi vipya vilihimizwa kufuata Ukristo
au Uislamu. Hii ilisababisha upotevu wa maarifa na desturi za kiutamaduni ambazo
kwa muda mrefu zilikuwa muhimu kwa mfumo wa kijamii wa jamii za Kitanzania.
Zoezi la 2.3
1. Bainisha athari zingine zilizoletwa na Ukristo nchini Tanzania.
2. Linganisha mfumo wa elimu ya jadi na mfumo wa elimu ya sasa.
3. Eleza mchango wa dini za jadi katika kulinda na kudumisha maadili ya
Kitanzania.
4. Fafanua umuhimu wa tiba za asili katika mazingira ya sasa ya Kitanzania.
Lugha: Kabla ya ukoloni, jamii za Kitanzania zilizungumza lugha za kiasili kama
vile Kimasai, Kisukuma, Kichaga, Kizigua, Kizaramo, Kidigo, Kimwera, Kitumbatu
na nyinginezo nyingi. Lugha hizi hazikuwa tu njia za mawasiliano, bali pia zilibeba
utamaduni, utambulisho, mila, desturi, miiko na kumbukumbu katika jamii iliyohusika.
Hata hivyo, mifumo ya elimu ya kikoloni ilileta mabadiliko makubwa kwenye lugha
za asili. Lugha kama Kiingereza kilianza kutumika kama lugha ya kufundishia shuleni,
hali iliyosababisha kupungua kwa matumizi ya lugha za asili. Moja ya athari kubwa
ilikuwa ni kushinikiza matumizi ya lugha za kikoloni hivyo kusababisha kupungua
kwa matumizi ya lugha za asili. Jamii zilianza kuwaona wasomi wanaozungumza
Kiingereza kama kipimo cha usomi na ustaarabu. Watu wasiojua kuandika na
kuzungumza Kiingereza walionekana kuwa si wasomi na wastaarabu. Usomi na
33
03/10/2024 18:15:10
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 33 03/10/2024 18:15:10
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 33

