Page 44 - Historia_Maadili
P. 44

Zoezi la          2.4



            1.  Fafanua athari  zilizosababishwa  na mwingiliano  kati ya wageni katika
               mitindo ya mavazi ya asili.

            2.  Eleza faida na changamoto za maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia katika
        FOR ONLINE READING ONLY
               kuyadumisha mavazi ya asili.

            3.  Umejifunza nini kutokana na athari za ukoloni katika mavazi ya Kitanzania?



          Mfumo wa utawala na sheria: Baada ya ujio wa utawala wa kikoloni, mifumo ya
          jadi ilibadilishwa na kuwekwa chini ya mamlaka ya kikoloni. Mabadiliko haya ya
          kiutawala yalileta maadili mapya kama vile utii kwa mamlaka ya kikoloni, muda
          wa kazi na kufuata sheria za kikoloni, ambazo mara nyingi zilikinzana na kanuni
          zilizowekwa za jamii za wenyeji. Msisitizo wa mamlaka ya mtu binafsi na udhibiti wa
          dola ya kikoloni ulivuruga utawala wa kijumuiya na wa maridhiano, ambao ulikuwa
          msingi wa jamii za Kitanzania.

          Kwa mfano, jamii za Kitanzania zilikuwa na sheria zao za kimila ambazo zilikuwa na
          mizizi katika mila, desturi na imani zao za kimaadili. Sheria hizi zilisimamia nyanja
          mbalimbali za maisha, zikiwemo ndoa, mali, mirathi, utatuzi wa migogoro na tabia
          za kijamii. Sheria hizi zilinyumbulika na kuendana na mahitaji na maadili ya jamii,
          zikiwa na lengo la kurejesha maelewano na kudumisha uhusiano mzuri ndani ya jamii.

          Hivyo basi, kuanzishwa kwa mifumo ya kisheria ya kikoloni kulileta mabadiliko
          makubwa ambayo mara nyingi yalikuwa magumu kutekelezwa na jamii. Sheria
          hizi zilitekelezwa na mahakama za kikoloni ambazo hazikuzingatia mila, desturi
          na taratibu za haki za jadi. Matokeo yake, sheria za kimila na desturi za jamii za
          Kitanzania ziliwekwa pembeni na hivyo kuvuruga mfumo wa maadili ya kijamii na
          kijadi kwa kuvunja mamlaka za viongozi wa jadi kama vile machifu na wazee wa
          kimila. Sheria hizi ni pamoja na mikataba rasmi, haki za umiliki wa ardhi na haki ya
          kuadhibu, ambazo mara nyingi zilikinzana na kanuni na sheria za kimila.

          Mifumo ya familia na jamii: Miundo ya kitamaduni ya familia katika jamii za
          Kitanzania ilijumuisha familia pana, zenye uhusiano wa kindugu na majukumu
          yaliyo wazi kwa kila mwanafamilia. Hata hivyo, kuja kwa ukoloni kuliathiri kwa kiasi
          kikubwa maadili na miundo ya familia na jamii hizo. Kwa mfano, uchumi wa kikoloni
          ulianzisha aina mpya za ajira kama vile kazi za ujira kwenye mashamba makubwa na
          migodi, ambazo mara nyingi zilihitaji wanaume kuhama kutoka maeneo ya vijijini
          kwenda mijini au maeneo ya kazi za mbali. Uhamaji huu ulivuruga majukumu ya
          kiutamaduni ya familia na hivyo wanawake walilazimika kubeba majukumu ya ziada
          katika kaya na jamii.


                                                  36




                                                                                        03/10/2024   18:15:11
   HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd   36
   HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd   36                                         03/10/2024   18:15:11
   39   40   41   42   43   44   45   46   47   48   49