Page 68 - Historia_Maadili
P. 68
masoko ya uhakika, kudai kupewa pembejeo na zana za kilimo, kupinga unyonyaji,
kunyang’anywa ardhi na kutozwa kodi kubwa ya mazao yao. Mfano wa vyama
hivi vya wakulima ni: Bukoba Buhaya Union (1924), Kilimanjaro Native Planters
Association (1925), Meru Citizens’ Union (1930), Sukuma Union (1930), Chama cha
Waluguru cha African Cotton Planters Association (1934), Nyakyusa Union (1937),
Buhaya Farmers’ Association (1937) na Pare Union (1949).
FOR ONLINE READING ONLY
Kwa upande wa Zanzibar, kulikuwa na jumuiya mbalimbali zilizoundwa na makundi
ya wakulima kwa malengo kama hayo ya wenzao kutoka Tanganyika. Kwa mfano,
Chama cha Wananchi wa Zanzibar cha Raia wa Sultani kilichojulikana kwa Kiarabu
kama Hizbu l’Watan l’Riaia Sultan Zanzibar, kwa kifupi HIZBU, kiliundwa na
wakulima wa Kiembe Samaki baada ya Vita ya Ng’ombe (Cattle Riot) mwaka
1951. Hata hivyo chama, pamoja na kuanzishwa na wakulima wa Kiembe Samaki,
hakikuanzishwa kama chama cha ushirika bali kama umoja wa wakulima.
Mbinu hii ya kuanzisha vyama vya ushirika haikuchangia tu kudai haki za wakulima,
bali pia ilichangia kwa kiasi kikubwa kuanzishwa kwa Sheria ya Ushirika nchini
Tanganyika mnamo mwaka 1932. Vyama hivi vilitoa watu mbalimbali ambao
baadaye walikuja kuwa viongozi wa kisiasa, kama Paul Bomani na Clement George
Kahama. Vilevile, vyama hivi vilipinga uamuzi wa serikali ya kikoloni ambao ulikuwa
unawakandamiza Watanganyika na Wazanzibari. Kwa mfano, vyama vya wakulima
wa Tanganyika vilipoungana na kukataa mapendekezo ya walowezi wa Kenya ya
kuanzisha shirikisho la Afrika Mashariki, ambalo lingewawezesha uhuru wa kutumia
ardhi na masoko katika nchi yoyote ya shirikisho hilo.
Vyama hivi vilichangia kwa kutoa fedha kwa TANU, kuunganisha na kuhamasisha
watu katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Pia, vyama vya ushirika
vilitoa elimu ya demokrasia kwa wanachama wao na kuwakumbusha umuhimu wa
kujikomboa kutoka mikononi mwa utawala wa kikoloni. Hivyo, pamoja na kudai haki
za wakulima, vilitumika kama mbinu ya kificho kudai haki za kisiasa, hasa wakati
wa harakati za kudai uhuru. Kielelezo 4.1 kinaonyesha picha ya George Kahama
na Paul Bomani, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa vyama vya ushirika
Tanganyika.
Kielelezo 4.1: Clement George Kahama (kushoto) na Paul Bomani (kulia)
60
03/10/2024 18:15:14
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 60
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 60 03/10/2024 18:15:14

