Page 67 - Historia_Maadili
P. 67
Zoezi la 4.1
1. Kwa kutumia mifano, eleza maana ya harakati za kupigania uhuru.
2. Kwa nini wananchi wa Tanganyika na Zanzibar walianzisha harakati za
kudai uhuru?
FOR ONLINE READING ONLY
3. Eleza kwa nini wakoloni walitumia sera za unyonyaji na ubaguzi wakati
wanatawala Tanganyika.
4. Tofautisha maadili ya kikoloni na yale ya jamii za Kitanzania wakati ukoloni
unaingia Tanganyika.
5. Je, ni athari gani zilizotokea kutokana na kudharauliwa kwa mila na desturi
za jamii za Kitanzania?
Mbinu zilizotumika kudai uhuru wa Tanganyika na Zanzibar
Kuna vipindi viwili muhimu vya harakati za wananchi katika kudai uhuru wa
Tanganyika na Zanzibar. Kipindi cha kwanza kilikuwa kati ya mwaka 1900 hadi
1944. Katika kipindi hicho, harakati ziliendeshwa na vikundi na vyama vya kijamii
na kidini (hasa kwa upande wa Tanganyika) katika maeneo machache tu. Kipindi
cha pili cha harakati hizi kilikuwa kati ya mwaka 1945 na 1964, ambapo harakati za
kudai uhuru zilikuwa na nguvu zaidi zikiendeshwa na vyama vya siasa. Katika kipindi
hiki, harakati hizo zilisambaa nchi nzima kutokana na mabadiliko yaliyotokana na
mchango wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia (1939 – 1945).
Harakati za kudai uhuru wa Tanganyika na Zanzibar zilitumia mbinu mbalimbali,
ikiwa ni pamoja na kuanzisha jumuiya, vyama na taasisi za kijamii za Waafrika.
Malengo ya kuanzishwa kwa jumuiya, vyama na taasisi hizo yalikuwa ni kutetea na
kudai haki za wafanyakazi, wakulima na wafanyabiashara. Kadiri muda ulivyoendelea,
jumuiya, vyama na taasisi hizo zilijihusisha na siasa na kuchangia sana katika harakati
za kudai uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
Vyama vya ushirika na wakulima
Chama cha ushirika ni muungano wa watu waliokubaliana kuendesha shughuli zao
za kiuchumi kwa pamoja ili kuinua hali zao za maisha. Shughuli hizi ni kama vile
kutafuta mahitaji yao ya chakula, elimu, uuzaji wa mazao yao na shughuli nyingine
za uchumi zinazoweza kuendeshwa kwa pamoja. Hata hivyo, jambo la muhimu
ni kuhakikisha kuwa watu hao wana mahitaji yanayofanana ya kupata huduma ya
shughuli yoyote ya kiuchumi iliyowafanya waanzishe chama.
Vyama vya wakulima vilianzishwa na wakulima wenyewe katika maeneo ambapo
mazao ya biashara yalilimwa. Vyama hivi vilijulikana kama vyama vya ushirika katika
sehemu mbalimbali za Tanganyika na Zanzibar. Baadhi ya malengo ya kuanzishwa
kwa vyama hivi yalikuwa ni pamoja na kudai bei nzuri ya mazao yao, kupata
59
03/10/2024 18:15:14
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 59
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 59 03/10/2024 18:15:14

