Page 70 - Historia_Maadili
P. 70
Kazi ya kufanya 4.2
Chagua chama kimojawapo cha ushirika au wafanyakazi kilichoshiriki harakati
za kudai uhuru wa Tanganyika na Zanzibar, kisha soma matini mbalimbali kupitia
FOR ONLINE READING ONLY
mtandao kuhusu chama hicho na andika maelezo yenye kurasa 2 kuhusu historia
na mchango wake katika harakati za kudai uhuru
Vyama vya wafanyabiashara
Vyama vya wafanyabiashara wa Kiafrika vilianzishwa nchini Tanganyika ili kuyalinda
na kuyatetea masilahi ya wafanyabiashara wa Kiafrika dhidi ya wafanyabiashara wa
kigeni. Baadhi ya madai yao yalijumuisha kupinga ubaguzi na unyanyasaji katika
masoko, kupinga kodi kubwa iliyokuwa ikitozwa na kuboresha mazingira ya kufanyia
biashara. Mfano wa vyama hivi ni African Commercial Association kilichoanzishwa
mwaka 1934 chini ya Erica Fiah. Hata hivyo, Fiah alikibadilisha chama hiki na
kukifanya Tanganyika African Welfare and Commercial Association mwaka 1936,
kisha kuanzishwa tena kama African Retail Traders’ Association mwaka 1937.
Kwa upande wa Zanzibar, kulikuwa na jumuiya mbalimbali za Wahindi, Waarabu na
Waafrika zilizoundwa ili kutetea masilahi yao ya kifedha na kibiashara. Mfano wa
jumuiya hizo ni Jumuiya ya Wahindi iliyoundwa mwaka 1910, ambayo ilianzishwa
ili kupambana na Waarabu waliokuwa wanadaiwa fedha nyingi na Wahindi baada ya
kufilisika kutokana na kufutwa kwa biashara ya utumwa Zanzibar. Pamoja na madai
haya, kulikuwa na harakati za chini kwa chini kuhusu masuala ya kisiasa.
Vyama vya kijamii viliendelea kukua mwaka hadi mwaka nchini Tanganyika na
Zanzibar na vilianzishwa vyama vyenye lengo la kuwaunganisha watu wa maeneo na
sekta mbalimbali. Mfano wa vyama hivi ni Tanganyika African Association (TAA),
kilichoanzishwa mjini Dar es Salaam mwaka 1929. Chama cha TAA kiliundwa
na watumishi wa serikali na baadaye kikazaa chama cha siasa kiitwacho TANU.
Rais wake wa kwanza alikuwa Cecil Matola na katibu wake alikuwa Abdulwahid
Kleist Sykes. Kufikia mwaka 1948, TAA kilikuwa na matawi makuu Dar es Salaam
na Dodoma. Zanzibar kulikuwa na African Association na Shirazi Association.
Jumuiya hizi mbili zilizoundwa Zanzibar zilikuja kuungana na kuunda chama cha
62
03/10/2024 18:15:15
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 62
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 62 03/10/2024 18:15:15

