Page 74 - Historia_Maadili
P. 74
na michezo kama vile kikundi cha taarabu cha Jipisheni. Kikundi hicho baadaye
kilipewa jina la Egyptian Music Club. Kikundi kingine cha taarabu kilikuwa ni
Al-Watan. Pamoja na taarabu kulikuwa vikundi vya lelemama ambavyo vilikuwa
na udugu na vikundi vya taarabu vya Al-Watan au Egyptian. Vikundi vyote hivi
vilitoa mchango mkubwa sana katika kuhamasisha watu kuiunga mkono TANU.
FOR ONLINE READING ONLY
Waliounganisha na kuviongoza vyama hivi vya wanawake na harakati za kudai uhuru
walikuwa Bibi Titi Mohamed na Bibi Hawa binti Maftah. Kielelezo 4.5 kinaonesha
picha ya Bibi Titi Mohamed akiwa jukwaani.
Kulikuwa pia na vyama vya wanawake kama Nujum ul Azhar na Egyptian Club
vilivyokuwepo mjini Tabora. Vyama hivi viliongozwa na wanawake kama Nyange
binti Chande na Zarura binti Abdulrahman na vilichangia sana kuipa TANU nguvu
katika Jimbo la Magharibi. Muziki na ujumbe uliokuwa katika nyimbo zilizotungwa
maalumu kwa ajili ya kuamsha ari ya wanachama wa TANU vilikuwa na athari
kubwa, hasa wakati ambapo serikali ya kikoloni ilimpiga marufuku Mwalimu Nyerere
kufanya mikutano ya hadhara.
Ili kukwepa marufuku hiyo, TANU iliandaa hafla za taarabu na Mwalimu Nyerere
alikuwa akikaribishwa kama mgeni rasmi. Mwalimu Nyerere alisimama kufungua
hafla hizo na, kwa kufanya hivyo, alisema maneno machache kuhusu harakati za
kudai uhuru. Kwa njia hii, ari ya kudai uhuru iliendelea kuwaka na Mwalimu Nyerere
aliweza kuwasiliana na wananchi. Vilevile, kupitia taarabu, TANU ilikusanya fedha
kwa ajili ya kuendeleza harakati za ukombozi.
Zoezi la 4.2
1. Je, ni kwa namna gani mbinu ya kuanzisha vyama vya kiraia ilisaidia
harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na Zanzibar?
2. Jadili nafasi ya vyombo vya habari katika harakati za kisiasa wakati wa sasa.
3. Fafanua nafasi ya vijana katika kudumisha uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
4. Eleza mchango wa vikundi na vyama vya kijamii na kidini katika kukukuza
demokrasia wakati wa sasa.
5. Pendekeza mikakati ya kudumisha uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
66
03/10/2024 18:15:16
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 66 03/10/2024 18:15:16
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 66

