Page 85 - Historia_Maadili
P. 85
Serikali ya Jamhuri ili kuwa na uwezo wa kuingia mikataba ya kimataifa kama nchi
huru na yenye mamlaka yake kamili. Sababu nyingine ya kuunda Jamhuri ilikuwa
ni kuwaondoa Wazungu katika nafasi za juu za uongozi na kuruhusu Watanganyika
kushika madaraka ya uongozi wa taifa lao. Baada ya Tanganyika kupata uhuru,
Waingereza walikuwa bado wameshikilia baadhi ya nafasi za uongozi na waliendelea
kutoa miongozo katika utawala wa nchi, hali iliyowafanya Watanganyika wajihisi
FOR ONLINE READING ONLY
kuwa bado wapo chini ya utawala wa kikoloni. Wananchi wa Tanganyika walitaka
kufanya uamuzi bila kuingiliwa na wakoloni, kwani viongozi wa serikali hawakuwa
na uhuru wa kufanya uamuzi wa kiutawala kabla ya kuwa Jamhuri.
Aidha, nchi kuwa Jamhuri kulilenga kuwapa uhuru wananchi na viongozi kujitawala
na kuharakisha maendeleo ya taifa. Jamhuri ilileta umoja na mshikamano, ikitokomeza
misingi ya ukabila na udini ambayo ilitumiwa na wakoloni kuwatenganisha
Watanganyika, hivyo kuwapa nafasi ya kujiletea maendeleo kwa kasi zaidi. Baada ya
Tanganyika kuwa Jamhuri, Mwalimu Nyerere aliunda baraza la kwanza la mawaziri,
kama baadhi yao wanavyoonekana katika Kielelezo 5.1.
Kazi ya kufanya 5.2
Tafuta taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ikiwamo mtandao ili kubainisha
majina ya mawaziri wa Baraza la Mawaziri la kwanza la Tanganyika mwaka
1961.
Kielelezo 5.1: Baraza la Kwanza la Mawaziri la Tanganyika mwaka 1961
77
03/10/2024 18:15:17
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 77
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 77 03/10/2024 18:15:17

