Page 90 - Historia_Maadili
P. 90
Aidha, uanzishwaji programu za mafunzo ya wahudumu wa afya na madaktari.
Hii ilijumuisha ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa tiba na wahudumu wa afya
waliokuwa wakipelekwa nje ya nchi kwa mafunzo ya juu. Vilevile, serikali ilijitahidi
kuleta vifaa tiba na dawa kutoka nje ya nchi ili kuongeza ubora wa huduma zilizokuwa
zinatolewa. Juhudi zote hizi ziliwezesha kuboresha hali ya afya kwa ujumla, kuweka
mfumo wa afya wakushughulikia changamoto mbalimbali za kiafya.
FOR ONLINE READING ONLY
Zoezi la 5.2
1. Eleza umuhimu wa elimu katika kujenga taifa lenye umoja, amani na
mshikamano mara baada ya uhuru.
2. Chambua mchango wa huduma za jamii katika kukuza uchumi wa nchi
mara baada ya uhuru.
3. Linganisha mikakati ya utoaji huduma za jamii mara baada ya uhuru na sasa.
Utamaduni na maadili
Utamaduni ni mfumo wa maisha unaojengwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja
hadi kingine kupitia malezi, elimu na mawasiliano ndani ya jamii. Unajumuisha
imani, maadili, mila na desturi, lugha, sanaa, muziki, mavazi, chakula na tabia ambazo
zinaainisha na kuunganisha kundi fulani la watu. Katika kipindi cha uhuru, utamaduni
ulikuwa na jukumu muhimu katika kuunda na kujenga taifa. Moja ya hatua kubwa
zilizochukuliwa na serikali katika kipindi hicho ilikuwa kuifanya lugha ya Kiswahili
kuwa lugha rasmi ya taifa. Wakati huo, Kiswahili hakikutumika tu kama chombo
cha mawasiliano, bali pia kama njia ya kuhifadhi na kueneza maarifa, maadili na
historia ya jamii.
Pia, serikali ilianzisha vyombo mbalimbali vya kusimamia sanaa na michezo ili
kulinda na kukuza utamaduni wetu. Ilianzisha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),
Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Bodi
ya Filamu Tanzania, Makumbusho ya Taifa na vyama mbalimbali vya kusimamia
michezo kama mpira wa miguu, pete, kikapu, ndondi na riadha.
Aidha, sanaa na muziki ni sehemu nyingine muhimu ya utamaduni iliyopewa uzito
kipindi hiki. Sanaa kama vile uchoraji, uchongaji, ngoma na nyimbo hutumiwa
kuelezea hisia, mawazo na historia ya jamii. Muziki ulitumika kuelezea maadili na
mapambano yaliyofanywa kulikomboa taifa. Vilevile, sanaa na muziki vilitumika
kuamsha hisia za umoja na fahari ya taifa. Wasanii na waandishi wa vitabu walihimizwa
kutumia kazi zao kuelimisha umma kuhusu ujenzi wa taifa. Bendi mbalimbali za
muziki zilianzishwa na nyingine kuimarishwa. Baadhi ya bendi hizo ni kama NUTA
Jazz Band (1964), Dar es Salaam Jazz Band, Kilwa Jazz Band, Morogoro Jazz Band,
82
03/10/2024 18:15:18
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 82
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 82 03/10/2024 18:15:18

