Page 86 - Historia_Maadili
P. 86
Kuanzishwa kwa sera ya Afrikanaizesheni: Hii ni sera iliyowapa madaraka
Watanganyika na Wazanzibari wazawa. Sera hii ililenga kutoa nafasi za uongozi na
ajira kwa wazawa ambazo awali zilikuwa zikishikiliwa na Wazungu na Waasia wakati
wa utawala wa kikoloni. Watanganyika na Wazanzibari wenye ujuzi walihamasishwa
kufanya kazi serikalini na katika mashirika ya umma.
Kuanzishwa kwa mifumo ya ulinzi na usalama: Ulinzi na usalama wa nchi ulikuwa
FOR ONLINE READING ONLY
ni suala lingine ambalo serikali iliweka mkazo katika kujenga taifa. Jitihada mbalimbali
zilianzishwa ili kuhakikisha nchi inakuwa salama. Mfumo wa ulinzi na usalama wa
taifa ulifayika kuanzia ngazi ya chini kupitia mfumo wa ubalozi wa nyumba kumi.
Huu ulikuwa ni mfumo wa kiulinzi uliowezesha kujua ni nani anaingia na kufanya
nini ndani ya nchi. Kwa kutumia mfumo huu, ilikuwa rahisi kuwabaini wageni na
wahalifu hivyo, kuimarisha ulinzi na usalama katika makazi ya wananchi wote.
Mfumo huu ulilenga kubaini shughuli, makazi na tabia za wananchi wote pamoja na
wageni wao. Pia, kwa wale waliokuwa wakisafiri walipaswa kuripoti kwa balozi ili
wajulikane walikotoka na wanakoelekea. Kila balozi alikuwa na jukumu la kusimamia
eneo lake na kutatua changamoto husika au kuziwasilisha kwa mamlaka zinazohusika
za serikali. Mfumo huu ulisaidia katika kulinda usalama, kujenga mshikamano,
kusimamia mila na desturi za Kitanzania na kutatua changamoto mbalimbali za
kijamii katika ngazi ya nyumba kumi.
Ili kuimarisha ulinzi na usalama, Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) liliundwa
mwaka 1964. Tanzania ilirithi jeshi la kikoloni
lililojulikana kama King’s African Rifles
(KAR), ambapo nafasi nyingi za juu zilikuwa
zikishikiliwa na wageni, yaani Wazungu
na Waasia. Mara baada ya uhuru, jeshi hili
lilibadilishwa jina na kuitwa Tanganyika
Rifles (TR) hadi mwaka 1964 lilipoanzishwa
JWTZ. Hii ni kufuatia maasi ya jeshi la TR
mwaka 1964 na serikali kuamua kuwafukuza
waasi wote kutokana na kukosa utii, uaminifu
na uzalendo. Brigedia Mirisho Sam Hagai
Sarakikya aliteuliwa kuwa mkuu wa majeshi Kielelezo 5.2: Brigedia Mirisho Sam
(Kielelezo 5.2). Hagai Sarakikya
Baada ya kuanzishwa kwa JWTZ, serikali ikawa makini kuteua na kuchagua watu
waliounda jeshi jipya. Kwa sehemu kubwa, jeshi hili liliundwa na vijana watiifu,
waadilifu na wazalendo kutoka Chama cha TANU na ASP. Hivyo, chini ya uongozi
wa Brigedia Sarakikya waliunda Jeshi la nchi kavu (infantry), jeshi la majini (navy)
na jeshi la anga (airforce). Pia Jeshi jipya lilianzisha shule za wapiganaji na vyuo
vya maofisa. Sarakikya aliongoza jeshi kuanzia 1964 hadi 1974.
78
03/10/2024 18:15:17
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 78 03/10/2024 18:15:17
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 78

