Page 83 - Historia_Maadili
P. 83
Sura ya Tano Ujenzi wa taifa baada
ya ukoloni
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Mara tu baada ya kupata uhuru, kilianza kipindi cha mpito kutoka katika
harakati za kudai uhuru hadi kuanzishwa kwa harakati mpya za ujenzi wa taifa
huru. Katika sura hii, utajifunza dhana ya ujenzi wa taifa, mifumo ya kiuchumi,
kisiasa, kijamii na kimaadili iliyojengwa kuanzia mwaka 1961 hadi 1966. Pia,
utajifunza mikakati na changamoto zilizokuwapo katika harakati za ujenzi wa
taifa. Umahiri utakaoujenga utakuwezesha kulinda na kuthamini juhudi za
ujenzi wa taifa zilizoanzishwa na waasisi wa taifa letu.
Fikiri
Hali ya taifa letu mara baada ya uhuru.
Dhana ya ujenzi wa taifa
Ujenzi wa taifa ni mchakato unaohusisha juhudi za pamoja za kuunda taifa jipya lenye
utambulisho wake kupitia mifumo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni,
unaozingatia haki, usawa na demokrasia. Katika taifa la Tanzania, mfumo huu
ulijengwa juu ya misingi ya kiitikadi, fikra, falsafa na maadili ya jamii za Kitanzania.
Harakati za ujenzi wa taifa zilikuwa muhimu kwa sababu ukoloni uliacha jamii
iliyogawanyika, yenye ukosefu wa miundombinu muhimu, rasilimali watu na pia
tofauti za kiuchumi na kijamii miongoni mwa wananchi. Harakati za ujenzi wa taifa
baada ya ukoloni zililenga kujenga umoja wa kitaifa, uchumi imara, demokrasia,
maadili na ustawi wa wananchi wote. Aidha, harakati hizi zililenga kuondoa mabaki
na kasumba za mifumo ya utawala wa kikoloni iliyokuwa imeigawa jamii katika
misingi ya rangi, kikabila, kidini na kikanda.
Mifumo iliyojengwa kati ya mwaka 1961 hadi 1966
Uhuru wa Tanganyika wa Desemba 9, 1961, pamoja na Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar ya Januari 12, 1964, yaliashiria mwanzo wa ujenzi wa mifumo mipya ya
75
03/10/2024 18:15:17
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 75 03/10/2024 18:15:17
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 75

