Page 81 - Historia_Maadili
P. 81
ushiriki wao katika kuanzisha na kusimamia vyama vya siasa. Kupitia vyama hivyo,
viongozi hawa walihamasisha uzalendo kwa kuwaongoza wanachama na hata
wananchi kudai uhuru na haki zao. Mbali na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
na Sheikh Abeid Amani Karume, kulikuwa na wazalendo wengine ambao nafasi
yao kubwa ilikuwa kufadhili harakati za uhuru kwa hali na mali. Miongoni mwao
walikuwemo John Rupia, Dossa Aziz, Abdulwahid Sykes na wengine. Uzalendo huu
FOR ONLINE READING ONLY
ulienea nchi nzima, ambapo watu walijitolea mali zao kusaidia harakati za uhuru.
Kwa mfano, Aikael Mbowe (Kilimanjaro), Hamisi Heri na Sadiki Patwa (Tanga),
pamoja na Suleiman Masudi Mnonji (Lindi).
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, pamoja na viongozi wengine, waliongoza chama
cha TANU kwa uzalendo hadi kufanikiwa kuikomboa Tanganyika kutoka kwa utawala
wa kikoloni. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitembelea sehemu mbalimbali
za Tanganyika katika juhudi za kuimarisha chama cha TANU. Kazi kubwa ilikuwa
kuwaandaa wananchi kwa ajili ya madaraka na uhuru. Pia, TANUkwa kushirikiana
na vyama vya wakulima na wafanyakazi, waliwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu
wa kujiunga na TANU ili kufanikisha kumng’oa mkoloni.
Hata hivyo, mwaka 1955, Julius K. Nyerere alitumwa na chama chake kwenda New
York, makao makuu ya Umoja wa Mataifa, ili Umoja huo uwashawishi Waingereza
kuipa Tanganyika uhuru wake. Mwaka 1957, Mwalimu Julius K. Nyerere aliteuliwa
kujiunga na Baraza la Kutunga Sheria - Legislative Council (LEGCO).
Haikuwa rahisi kwa TANU kusonga mbele bila vikwazo. Waingereza waliwakataza
watumishi wa serikali kujiunga na vyama vya siasa. Pia, mikutano ya hadhara ilipigwa
marufuku na matawi ya TANU yalifungwa katika baadhi ya maeneo kwa lengo la
kuidhoofisha TANU. Hata hivyo,
chama hiki kiliendelea kusonga
mbele na kushinda kwenye
uchaguzi wa mwaka 1958/1959.
Katika uchaguzi wa mwaka
1960, TANU ilishinda na kupata
wajumbe wengi katika Baraza
la Kutunga Sheria. Ushindi huo
uliwaharakisha Watanganyika
kupata uhuru wao mapema. Uhuru
ulipatikana tarehe 9 Desemba 1961.
Kielelezo 4.9 kinaonesha picha ya Kielelezo 4.9: Wananchi wakisherehekea uhuru wa
wananchi wakisherehekea uhuru Tanganyika mwaka 1961
wa Tanganyika.
73
03/10/2024 18:15:16
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 73 03/10/2024 18:15:16
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 73

