Page 91 - Historia_Maadili
P. 91
Cuban Marimba Band na Jamuhuri Jazz Band. Bendi hizi zilivutia mashabiki wengi
kwa mtindo wa muziki wa rumba na cha-cha-cha. Mlimani Park Orchestra (Sikinde)
ilianzishwa mwaka 1978, lakini chimbuko lake lilikuwa katika miaka ya 1960 na
baadaye ikawa mojawapo ya bendi kubwa sana nchini. Kielelezo 5.3 kinaonesha
baadhi ya waimbaji wa bendi ya muziki ya NUTA wakiwa jukwaani.
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo 5.3: NUTA Jazz Band
Kazi ya kufanya 5.4
Kwa kutumia mtandao au maktaba mtandao, soma matini mbalimbali na chunguza
mchango wa lugha ya Kiswahili katika kujenga utambulisho wa taifa mara baada
ya uhuru. Baada ya uchunguzi andika ripoti fupi kwa maneno yasiyozidi ukurasa
mmoja.
Zoezi la 5.3
1. Je, ni kwa namna gani sanaa na muziki vinaweza kuendelea kutumika kama
nyenzo za kuyajenga maadili na uzalendo katika Tanzania ya sasa?
2. Eleza nafasi ya sanaa katika kuleta maendeleo ya jamii.
3. Eleza nafasi ya Kiswahili katika kuuendeleza na kuudumisha utamaduni wa
Mtanzania kwa kizazi cha sasa.
83
03/10/2024 18:15:18
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 83
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 83 03/10/2024 18:15:18

