Page 98 - Historia_Maadili
P. 98
Aina ya pili ni mapinduzi ya kijeshi. Mapinduzi haya hufanywa na jeshi kwa lengo
la kuondoa utawala uliopo madarakani kwa kutumia mapigano au mbinu za kijeshi.
Mfano wa mapinduzi ya aina hii ni yale yaliyotokea Misri yakiongozwa na Kanali
Gamal Abdel Nasser dhidi ya Mfalme Farouk I mwaka 1952, mapinduzi ya Mengistu
Haile Mariam wa Ethiopia dhidi ya Haile Selassie mwaka 1974, mapinduzi ya Jenerali
Iddi Amin Dada wa Uganda dhidi ya Rais Milton Obote mwaka 1971 na mapinduzi
FOR ONLINE READING ONLY
ya Libya chini ya Kanali Muammar Gaddafi dhidi ya Mfalme Idris mwaka 1969.
Zoezi la 6.1
1. Eleza sababu zilizosababisha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
2. Fafanua namna uzalendo na ujasiri ulivyochangia kufanyika kwa Mapinduzi
ya Zanzibar.
3. Jadili umuhimu wa kuyalinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Kazi ya kufanya 6.1
Umeteuliwa kushiriki katika mdahalo wenye mada isemayo “Mapinduzi ilikuwa
ndio njia pekee ya Wazanzibari kujikwamua kutoka katika ukoloni.” Soma vitabu
na matini mbalimbali kisha andaa dondoo utakazotumia wakati wa mdahalo.
Chimbuko la Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Zanzibar ilikuwa chini ya utawala wa kisultani hadi mwaka 1890. Kama ilivyotajwa
awali, Sultani Seyyid Saidi alikuwa sultani wa kwanza kuongoza dola mbili, yaani
Oman na Zanzibar, akiifanya Zanzibar kuwa makao makuu ya himaya hizo. Sultani
Seyyid Said alihamia Zanzibar mwaka 1840 akitokea Muscat, Oman. Mnamo mwaka
1890, Zanzibar iliwekwa chini ya utawala wa Waingereza na ikatambulika kama
Mahamia ya Uingereza au “British Protectorate.” Katika hali hiyo, utawala wa sultani
ulitumiwa na Waingereza katika kuitawala Zanzibar. Hali hii ilisababisha mgawanyiko
mkubwa kati ya Waarabu wachache, ambao walikuwa na nguvu kubwa za kisiasa
na kiuchumi na Waafrika walio wengi ambao hawakuwa na nguvu zozote zaidi ya
umasikini na kutumikishwa na Waarabu pamoja na wageni wengine wakiwemo
Waingereza na Waasia.
90
03/10/2024 18:15:19
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 90
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 90 03/10/2024 18:15:19

