Page 100 - Historia_Maadili
P. 100
yalifanyika mapinduzi rasmi Zanzibar chini
ya uongozi wa mwanamapinduzi Sheikh Abeid
Amani Karume, ambaye aliiongoza Zanzibar
kuanzia mwaka 1964 hadi alipouawa tarehe 7
April1972. Kielelezo 6.1 kinaonesha aliyekuwa
FOR ONLINE READING ONLY
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Sheikh Abeid Amani Karume. Kielelezo 6.1: Sheikh Abeid Amani
Karume
Zoezi la 6.2
1. Fafanua sababu za kihistoria zilizosababisha Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar mwaka 1964.
2. Eleza mchango wa Sheikh Abeid Aman Karume kwenye Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar.
3. Eleza mchango wa vijana katika kufanikisha Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar.
Sababu za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Kama ilivyoelezwa hapo awali, Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalikuwa matokeo
ya upendeleo uliokuwepo tangu enzi za ukoloni, upendeleo ambao ulisababisha
ubaguzi mkubwa katika sekta mbalimbali na kuwafanya Waafrika kuwa duni na
wanyonge. Ubaguzi huu ulikuwa pigo kubwa kwa Waafrika kisiasa, kiuchumi na
kijamii. Hali hii iliwapa Waafrika msukumo na hamasa ya kupigania haki na usawa
katika nyanja za siasa, uchumi na utamaduni.
Wakati wa harakati za ukombozi wa Zanzibar, mfumo wa kimaadili ulikuwa
umeathiriwa sana na mazingira ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Tabaka la Waafrika
lilikuwa limebaguliwa na wakoloni kwa muda mrefu katika nyanja zote. Hivyo, Kamati
ya vijana jasiri na shupavu iliundwa mapema hata kabla ya uhuru wa bandia wa tarehe
10 Desemba 1963. Lengo la kamati hiyo lilikuwa ni kuratibu kwa usiri wa hali ya juu
suala zima la mapinduzi. Vijana hawa walifanya maandalizi yote na mnamo tarehe
92
03/10/2024 18:15:19
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 92 03/10/2024 18:15:19
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 92

