Page 6 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 6
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Dibaji
Kiongozi hiki kimeandaliwa mahususi kwako mwalimu wa Fasihi ya
FOR ONLINE READING ONLY
Kiswahili Kidato cha Tano. Kiongozi hiki kimeandaliwa kulingana
na kitabu cha Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kitabu cha
Mwanafunzi Kidato cha Tano cha mwaka 2024. Lengo kuu la kiongozi
hiki ni kukupa mwalimu mbinu na maarifa ya kufundisha somo la Fasihi
ya Kiswahili katika kidato cha tano. Katika ngazi hii, mwanafunzi
anatakiwa aweze kumudu vizuri Fasihi ya Kiswahili ili aweze kutumia
maarifa yake katika kuchambua, kutathmini, kubuni na kutunga kazi
mbalimbali za kifasihi kulingana na miktadha mbalimbali.
Lugha iliyotumika ni ya kifasihi na inaendana na kiwango cha wajifunzaji.
Aidha, mbinu mbalimbali za ufundishaji zimependekezwa. Hata hivyo,
una uhuru wa kubuni mbinu nyingine kulingana na mazingira, idadi na
uwezo wa wanafunzi wako ili kuleta ufanisi katika ujifunzaji. Katika
mchakato wote wa ufundishaji na ujifunzaji, washirikishe wanafunzi
katika kutenda shughuli mbalimbali za ujifunzaji zilizoandaliwa katika
Kitabu cha Mwanafunzi. Lengo la kufanya hivyo ni kujenga umahiri
utakaomwezesha mwanafunzi kuwa kitovu cha ujifunzaji.
Jifunze zaidi kupitia Maktaba Mtandao. https://ol.tie.go.tz/videos
Taasisi ya Elimu Tanzania
vi Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 6
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 6 23/06/2024 17:48