Page 11 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 11
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
mwanafunzi anashiriki kikamilifu katika majadiliano pamoja
na kuandika nukuu ya kile wanachokijadili.
(ii) Waongoze wanafunzi katika kufanya matembezi msambao kwa
lengo la kupeana maarifa waliyoyajadili katika vikundi vyao ili
FOR ONLINE READING ONLY
kupata maarifa mapya. Katika kila kikundi abaki mwanafunzi
mmoja ili awaelekeze wanafunzi watakaotoka katika vikundi
vingine. Baada ya matembezi hayo, wanafunzi warudi katika
vikundi vyao vya awali na kupeana maarifa mapya. Rekebisha
dosari zinazojitokeza katika majadiliano yao.
(iii) Hitimisha na kutoa mrejesho kuhusiana na shughuli husika.
(iv) Waongoze kufanya maswali ya tamrini yaliyomo kwenye
Kitabu cha Mwanafunzi.
(v) Kusanya kazi zao, kisha sahihisha na kutoa mrejesho.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 1.6 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi aeleze kwa mifano ubora na udhaifu
unaojitokeza katika nadharia za chimbuko la fasihi.
Majibu ya maswali ya tamrini yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Kiongozi cha Mwalimu 5
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 5 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 5