Page 13 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 13
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Mahitaji: Chati/ mti wenye tanzu za fasihi simulizi na fasihi andi-
shi, ramani ya dhana, nyimbo, mashairi, na maigizo ya-
liyorekodiwa, matini na makala za magazetini, kamusi,
chati ya alama za LAT
FOR ONLINE READING ONLY
Somo la 1: Tanzu na vipera vya fasihi simulizi na fasihi andishi
Shughuli ya 2.1
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kubungua bongo kuhusu matumizi ya
fasihi kama nyenzo ya kuwasilisha mawazo katika miktadha
mbalimbali kisha tumia kibaofumbo ili kupata baadhi ya
wanafunzi kujibu maswali hayo. Rekebisha upungufu
unaojitokeza.
(ii) Waongoze wanafunzi kutumia vyanzo vya mtandaoni au
maktabani kusoma matini kuhusu shughuli ya 2.1 iliyomo
kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
(iii) Waelekeze wanafunzi kukaa katika jozi au vikundi ili kujadili
shughuli ya 2.1 iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha
kuwasilisha wawasilishe kazi zao walizojadili katika vikundi
kwa ajili ya majadiliano zaidi.
(iv) Rekebisha upungufu unaojitokeza wakati wa uwasilishaji ili
kuleta uelewa wa pamoja.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 2.1 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi aeleze kwa mifano kuhusu dhana ya
tanzu na vipera kwa kuongozwa na maswali yaliyopo katika Kitabu
cha Mwanafunzi. Majibu ya shughuli hii yanaweza kueleza tofauti kwa
kuzingatia vigezo vya utunzi, uwasilishaji na uhifadhi.
Kiongozi cha Mwalimu 7
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 7 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 7