Page 9 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 9

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari


                  zaidi. Hakikisha kila mwanafunzi anashiriki katika uwasilishaji
                  kwa kutoa mawazo yake na au kuuliza maswali.

              (ii) Rekebisha  upungufu unaojitokeza  wakati  wa uwasilishaji
           FOR ONLINE READING ONLY
                  darasani kuhusu mitazamo ya dhana za fasihi.
           Majibu


           Majibu ya shughuli ya 1.3 yatatokana  na uelewa wa mwanafunzi.
           Katika shughuli hii, mwanafunzi aeleze mitazamo ya dhana ya fasihi
           kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali.

           Shughuli ya 1.4

           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze wanafunzi kukaa katika vikundi na kujadili shughuli
                  ya 1.4 iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha chagua
                  baadhi vikundi vitakavyowasilisha hoja hizo kwa niaba ya
                  vikundi vingine. Kumbuka kuchanganya  vikundi hivyo ili
                  wanafunzi wapeane maarifa mbalimbali. Rekebisha upungufu
                  unaojitokeza wakati wa uwasilishaji.

             (ii)  Waongoze  wanafunzi  kufanya  zoezi  la  1.1  lililomo  kwenye
                  Kitabu  cha  Mwanafunzi  kisha  kusanya  kazi  za  wanafunzi,
                  sahihisha na kutoa mrejesho.

           Majibu

           Majibu ya shughuli ya 1.4 yatatokana  na uelewa wa mwanafunzi.
           Katika shughuli hii, mwanafunzi aeleze ubora na upungufu wa kila
           mtazamo wa dhana ya fasihi kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali.

           Majibu ya zoezi lililomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi yatatokana
           na uelewa wa mwanafunzi na maswali husika.






                 Kiongozi cha Mwalimu                                     3
                    Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   3     23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   3
   4   5   6   7   8   9   10   11   12   13   14