Page 10 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 10

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari



             Somo la 2: Nadharia za chimbuko la fasihi



           Shughuli ya 1.5
           FOR ONLINE READING ONLY
           Hatua za ufundishaji
             (i)   Waongoze wanafunzi kusoma matini mbalimbali zinazopatikana
                  mkondoni au maktabani  zinazohusiana  na shughuli ya 1.5
                  iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi. Hakikisha kila
                  mwanafunzi anashiriki katika kupakua na kuchambua matini
                  hizo.

             (ii)  Waelekeze  wanafunzi  kukaa  katika  vikundi  ili  kuchambua
                  matini  za  nadharia  za  chimbuko  la  fasihi.  Hakikisha  kila
                  mwanafunzi anashiriki katika majadiliano.

             (iii)  Waongoze  wanafunzi  kufanya uwasilishaji,  chagua  vikundi
                  vichache  kuwasilisha  nadharia  za  chimbuko  la  fasihi
                  walizozichambua  kwa niaba  ya  wengine.  Hakikisha  kila
                  mwanafunzi anashiriki kwa kutoa mawazo na kuuliza maswali
                  wakati wa uwasilishaji. Rekebisha upungufu unaojitokeza.
             (iv)  Hitimisha kwa kutoa maelezo yanayohusiana na shughuli
                  husika.

           Majibu

           Majibu ya shughuli ya 1.5 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi. Katika
           shughuli hii, mwanafunzi aeleze kwa mifano nadharia za chimbuko la
           fasihi kwa kutumia vyanzo mbalimbali atakavyokuwa amevisoma au
           kujadili darasani.

           Shughuli ya 1.6
           Hatua za ufundishaji
             (i)   Waongoze wanafunzi kukaa katika vikundi ili kujadili shughuli
                  ya 1.6 iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi. Hakikisha kila


              4                                        Kiongozi cha Mwalimu
                                                          Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   4
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   4     23/06/2024   17:48
   5   6   7   8   9   10   11   12   13   14   15