Page 15 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 15

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari


                   kila mwanafunzi anashiriki na kuchukua dondoo za hoja
                   zinazojadiliwa.  Rekebisha dosari zinazojitokeza  katika
                   majadiliano.
             (iii)  Waongoze wanafunzi kufanya uwasilishaji. Chagua wanafunzi
           FOR ONLINE READING ONLY
                   wachache kuwasilisha hoja zao. Hakikisha kila mwanafunzi
                   anashiriki kikamilifu. Rekebisha dosari zinazojitokeza katika
                   uwasilishaji.

           Majibu

           Majibu  ya  shughuli  ya  2.3  yatatokana  na  uelewa  wa mwanafunzi.
           Katika shughuli hii, mwanafunzi afafanue kwa mifano semi na vipera
           vyake kama vile methali, misemo, mizungu na vitendawili. Ufafanuzi
           huo uzingatie umuhimu wa kila kipera katika jamii.

           Shughuli ya 2.4

           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze wanafunzi kukaa katika jozi ili kutumia maktaba au
                   maktaba mtandao na vyanzo vingine kusoma matini zinazohusu
                   shughuli  ya  2.4 iliyomo  kwenye  Kitabu  cha  Mwanafunzi.
                   Hakikisha kila mwanafunzi anashiriki kikamilifu kupakua na
                   kuchambua matini hizo huku akichukua dondoo muhimu.

             (ii)  Waelekeze wanafunzi kuandaa na kutunga mjadala unaohusu
                   ushairi simulizi wa Kiswahili na vipera vyake. Hakikisha kila
                   mwanafunzi anashiriki kikamilifu kwa kuchangia hoja katika
                   mjadala huo.

           Majibu

           Majibu  ya  shughuli  ya  2.4  yatatokana  na  uelewa  wa mwanafunzi.
           Katika shughuli hii, mwanafunzi afafanue kwa mifano maana, sifa na
           vipera vya ushairi simulizi. Mwanafunzi aeleze namna ushairi simulizi
           unavyotofautiana na ushairi andishi.



                 Kiongozi cha Mwalimu                                     9
                    Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   9     23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   9
   10   11   12   13   14   15   16   17   18   19   20