Page 20 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 20
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Shughuli ya 2.12
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kutumia vyanzo mbalimbali kusoma
FOR ONLINE READING ONLY
hadithi fupi kisha kukaa katika jozi au vikundi ili kufanya
shughuli ya 2.12 iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
(ii) Waulize wanafunzi maswali kuhusiana na shughuli ya 2.12 ili
kuleta uelewa wa pamoja.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 2.12 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi aeleze dhana na historia ya tamthiliya.
Shughuli ya 2.13
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kukaa katika vikundi kutumia vyanzo
vya maktabani kusoma tamthiliya na kufanya shughuli ya 2.13
iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha kuwasilisha
kazi zao. Hakikisha kila mwanafunzi anashiriki kikamilifu.
Rekebisha upungufu unaojitokeza wakati wa uwasilishaji
Majibu
Majibu ya shughuli ya 2.13 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi
kutokana tamthiliya atakazozichambua. Katika shughuli hii,
mwanafunzi aeleze aina ya tamthiliya alizozichambua.
Shughuli ya 2.14
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kutumia vyanzo mbalimbali kusoma
riwaya kisha kukaa katika vikundi na kujadili shughuli ya 2.14
14 Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 14
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 14 23/06/2024 17:48