Page 24 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 24
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Somo la 5: Mchango wa fasihi simulizi na fasihi andishi katika
maendeleo ya jamii
Shughuli ya 2.19
FOR ONLINE READING ONLY
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kubungua bongo kwa kufanya shughuli
ya 2.19 iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha
chagua wanafunzi wachache wajibu maswali utakayowauliza.
Hakikisha kila mwanafunzi anashiriki kwa kujibu au kuuliza
maswali yanayochochea mjadala. Rekebisha upungufu
unaojitokeza wakati wa uwasilishaji.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 2.19 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi akusanye methali tano (5) zinazoonya
kuhusu utovu wa nidhamu na misemo mitano (5) inayohamasisiha
ushirikiano katika maisha. Pia, mwanafunzi aeleze umuhimu wa semi
hizo katika maendeleo ya jamii.
Shughuli ya 2.20
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kukaa katika vikundi na kujadili shughuli
ya 2.20 iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi. Hakikisha
kila mwanafunzi anashiriki kikamilifu katika majadiliano.
(ii) Waelekeze wanafunzi kufanya uwasilishaji kwa kuwauliza
maswali na wanafunzi wajibu kuhusu mchango wa fasihi
katika maendeleo ya jamii. Rekebisha upungufu unaojitokeza
ili kuleta uelewa wa pamoja.
18 Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 18
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 18 23/06/2024 17:48